Kuna Dokta Mbwambo, yuko KCMC na anaclinic yake Moshi mjini karibu na TRA.
Kufa ni mipango ya mungu.Ni kweli dokta mbwambo ni urologist mzuri, amefanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka 20, na ndiyo among waanzilishi wa chuo cha urology KCMC.
Tatizo la mzee japo sijamuona, ila kwa umri wake huenda ikawa aidha Benign prostatic hyperplasia (hii ni salama zaidi) au cancer of the prostate(hatari zaidi).
Sasa ukiogopa kumpeleka kwa madaktari itashindikana kujua kama huo uvimbe wa kwenye tezi la kiume(prostate) ni kansa au la.
Mara nyingi sio wote wanaofanyiwa operesheni ya kufungua tumbo, wengine wanafanyia operesheni ndogo ya kuzibua njia ya mkojo (TURP) ambayo inatumia dakika chache na mgonjwa kesho yake anatembea na anakula kama kawaida.
ila kwa umri wake, (na uwezekano wa kuwa kansa kutokana na umri), kuna uwezekano wa kufanyiwa operesheni kubwa ili tezi lote litolewe na kufanyiwa uchunguzi wa kina (histopathology).
Kwa hiyo nakushauri umpeleke hospitali mapema iwezekanavyo.Ukiweza nenda kwa mbwambo au KCMC.
kama uko mwanza, bugando wanafanya operesheni hizi, bahati mbaya daktari ni mmoja, na wagonjwa walivyojaa wodini, wote wanasubiri zamu yao.