Msaada juu ya dawa ya kibofu cha mkojo wa mtu mzee

Msaada juu ya dawa ya kibofu cha mkojo wa mtu mzee

bishankara

Senior Member
Joined
Feb 21, 2012
Posts
140
Reaction score
8
Madaktari naomba mnisaidie dawa ya kibofu cha mkojo kwa mzee wangu. Anakojoa kwa shida sana. Kuna ushauri alikuwa amepata kuwa inabidi afanyiwe upasuaji. Lakini cha kusikitisha ni kwamba, wazee anaowajua walokuwa na tatizo kama lake walipofanyiwa upasuaji walikufa. Naomba kwa mwenye kujua dawa ambayo ni alternative na upasuaji aniambie nimnunulie mzee. NB: Ni mzee wa zaidi ya miaka 65.
 
Mkuu kama madaktari wamekwambia upasuaji ndo suluhisho kwa nn usimshauri afanyiwe tu.wazee wanateseka sana,mm baba yangu alikuwa na hiyo shida mbona alifanyiwa upasuaji mwaka juzi hadi leo mzima na ana miaka zaidi ya hiyo 65.vinginevyo atatumia mpira tu(catheter).
 
Mkuu kama madaktari wamekwambia upasuaji ndo suluhisho kwa nn usimshauri afanyiwe tu.wazee wanateseka sana,mm baba yangu alikuwa na hiyo shida mbona alifanyiwa upasuaji mwaka juzi hadi leo mzima na ana miaka zaidi ya hiyo 65.vinginevyo atatumia mpira tu(catheter).

Asante kwa ushauri
 
Kuna Dokta Mbwambo, yuko KCMC na anaclinic yake Moshi mjini karibu na TRA.
 
Kuna Dokta Mbwambo, yuko KCMC na anaclinic yake Moshi mjini karibu na TRA.
Kufa ni mipango ya mungu.Ni kweli dokta mbwambo ni urologist mzuri, amefanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka 20, na ndiyo among waanzilishi wa chuo cha urology KCMC.
Tatizo la mzee japo sijamuona, ila kwa umri wake huenda ikawa aidha Benign prostatic hyperplasia (hii ni salama zaidi) au cancer of the prostate(hatari zaidi).
Sasa ukiogopa kumpeleka kwa madaktari itashindikana kujua kama huo uvimbe wa kwenye tezi la kiume(prostate) ni kansa au la.
Mara nyingi sio wote wanaofanyiwa operesheni ya kufungua tumbo, wengine wanafanyia operesheni ndogo ya kuzibua njia ya mkojo (TURP) ambayo inatumia dakika chache na mgonjwa kesho yake anatembea na anakula kama kawaida.
ila kwa umri wake, (na uwezekano wa kuwa kansa kutokana na umri), kuna uwezekano wa kufanyiwa operesheni kubwa ili tezi lote litolewe na kufanyiwa uchunguzi wa kina (histopathology).
Kwa hiyo nakushauri umpeleke hospitali mapema iwezekanavyo.Ukiweza nenda kwa mbwambo au KCMC.
kama uko mwanza, bugando wanafanya operesheni hizi, bahati mbaya daktari ni mmoja, na wagonjwa walivyojaa wodini, wote wanasubiri zamu yao.
 
kwa dar hosp nzuri kwa ugonjwa huo ni ipi??
 
Mzee wako hadi sasa anaendeleaje!pia ana mdagan ana tatzo hilo?kifupi tatzo hilo linatibika kwa100%.usibabaike chakufanya wasiliana nami kwa 0759217720.Ni wazee wengi wanapona zaidi hata ya umri wa mzee wako.
 
Back
Top Bottom