Msaada juu ya hizi fursa.

joshydama

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2016
Posts
4,623
Reaction score
5,039
Habari wakuu!

Ni kwamba kati ya hizi fursa ni ipi ni rahisi kuendesha na inatengeneza faida nzuri.

i) uuzaji wa kitimoto

ii) uuzaji wa matunda

iii) kukopesha watu hela ( watumishi wa serikali mfano walimu n.k)


Karibuni kwa maoni yenu.
 
Kuuza kitimoto inatoka sana hasa maeneo yenye bar,,,

Kabla ya kuanza kuuza fanya utafiti kwanza maana maeneo yanatofautiana kutokana na wateja wa sehemu husika,

Lakini biashara hiyo inatokana sana kuna watu wanaifanya na inawalipa sana,

Fanya utafiti kwa kuzunguka maeneo wanayouza na uongee na wauzaji utagundua kitu,
 
Habari wakuu!

Ni kwamba kati ya hizi fursa ni ipi ni rahisi kuendesha na inatengeneza faida nzuri.

i) uuzaji wa kitimoto

ii) uuzaji wa matunda

iii) kukopesha watu hela ( watumishi wa serikali mfano walimu n.k)


Karibuni kwa maoni yenu.
upo mkoa gani
 
Ahsante Mkuu!
 
Kila kitu ni kizuri kutegemea na mazingira na uzoefu wako kwenye mazingira husika. Mfano kukopesha kunategemea sana na ufahamu na ujirani na wa husika maana wengine huwa wanashida kulipa hivyo huenda wakakurudisha nyuma sana. Lakini Fanya analysis ya kutosha. Kitimoto inauzika sana ukipata sehemu yenye bar, ni advantage sana na kuweza kuwa popular very good one...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…