joshydama
JF-Expert Member
- May 10, 2016
- 4,623
- 5,039
Inabidi hao ndugu waende mahakamani wakiwa na sababu za msingi au zinazofaa kumuondoa huyo msimamizi.Kama taratibu zote zimefanyika na mahakama ikatoa hati ya usimamizi kwa aliyeteuliwa/chaguliwa lakini Baada ya miaka miwili au mitatu ikatokea labda ndugu wengine hawakuridhika inakuwaje hapo?
Hivyo basi mahakama lazima iridhike na sababu walizotoa na kama itaona sawa kumuondoa msimamizi ili kuokoa mali zilizoachwa na marehemu, hakika lazima itafanya hivyo.
Ingawa mahakama huwa inapewa utashi mkubwa sana wa kumuondoa msimamizi yani unaweza peleka hizo sababu na bado zikapigwa chini na mahakama.