Uhaligani bro,
Wahenga walisema hakuna swali la ujinga au mbaya ILA jibu.
Masomo tunayopata darasani pamoja na matokeo ya mitihani ni ishara na vipima ujuzi tu. Umuhimu hasaa wa yale masomo ni kumwezesha mtu kuyaelewa maisha na ulimwengu, ni darubini ya kuyavuta mambo na matukio yakawa jaribu nawe kikuyaelewa. You can apply your knowledge BUT you can't employ it.
Swali la kujiuliza mdogo wangu ni, unafurahia kufanya kitu kipi kwa maisha. Kitu/fani ambayo itakuletea furaha na kukuridhisha hata bila kipato na heshima hata bila umaarufu. Hapo basi utaweza kuishi maisha mazuri na ya furaha. Ila wengi wanataka pesa, mali na sifa/wanawake(wanaume) na hizi hazihitaji fani au course kuzipata.