Msaada juu ya kuletewa kreti za bia na soda

INSIDER MAN

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2018
Posts
2,005
Reaction score
19,579
Habari za jion wana jeifu.

Ndugu zangu nimeamua nimfungulie mama watoto biashara ili asikae home kizembezembe nae ajifunze kutafuta hela.

Biashara ni kuuza vinywaji kwa jumla kama bia, soda, juice, maji nk. Bia tumetarget za local na baadhi za imported kama heineken, savanna nk. Kadri biashara itakapokuwa inakwenda vzr tutaanza kuongeza na vinywaji vingine.

Msaada naomba kujua ili TBL wakuletee kreti za bia dukani kwako unatakiwa uanze na kreti ngapi? Na kwa upande wa kampuni ya cocacola na pepsi na wenyewe wanataka uanze na kreti ngapi?

Ni hayo tu naombeni mwongozo kwa wale wajuzi na wenye uzoefu na hii biashara.
 
Ili tbl wakuletee bia hapo unahitaji uwe na uwezo wa kuchukua kreti kuanzia 300.
Ili kampuni za soda zilete inabidi umendee tu kilori cha soda kikiwa kinapita. Au ukatafute namba zao.

Shukran kwa mwongozo mkuu kama unachukua kreti 50. Hapa nafanyaje ili niuze kwa jumla nipate faida kidogo
 
Tbl wanatoa bia toka kiwandani kwao kwenda kwenye distribution centre, awa wanauzia stockist ambao hawawezi kuagiza gari kubwa au crate nyingi. Ili uweze kununua kiwandani utaitaji uchukue mzigo mkubwa, pia uwe na account

Kwa vile unaanza itabidi ununue kwa dc/stockists katika bei elekezi, ndipo wewe utaendelea na process za uuzaji.

Nafikiri soda nao wanafanya hivyo hivyo pia kama nakusoea ntarekebishwa
 
Uko sahihi kabisa. Kwa coca cola inabidi amjue local authorized distributor kwa kuwa anaanza na mzigo kidogo ndo ampe mzigo kama stockist. KwsaPepsi atege magari yao yanayopita barabarani wamshushie kwake dukani kabisa kama panafikika na gari. Note that: Kama hana makreti matupu itabidi anunue kwao kwa gharama ya 10000tsh kwa kila kreti tupu. Na kwa bia aulizie alipo agent wao mkubwa wa karibu atamshushia hadi dukani kwake. The same kwa watu wa maji na juisi.
 

Ahsante kwa mwongozo mkuu [emoji1666]
 
Asante kwa ufafanuzi.Naomba kujua bei ya kreti ya soda kwa bei ya jumla,ambayo kiwanda kitamuuzia agent.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…