najibu kwa ufupi maswali ninayoulizwa kwa simu kuhusu business names registration
swali nahitaji kuambatanisha kitu gani kama nataka kusajili jina la biashara?
jibu hauitaji kuambatanisha doc yoyote katika form ya kusajili jina la biashara, ila kuna taarifa kama ,jina ama majina unayopendekeza kutumia,box no, house no/block no mtaa,wilaya na mkoa wa eneo unaloishi na unalotegemea kufannyia shughuli zako za biashara, jina la mtu ambaye ndio mwenye hiyo biashara n.k.
swali utaratibu wa kusajili kikundi brela ukoje,je katiba ya kikundi inahitajika?
jibu kusajili kikundi brela haiitaji kuambatanisha katiba ya kikundi,ila form inayotumika kusajili patnership business ndio hutumika kujaza info za kikundi, na watu wa hicho kikundi wasizidi ishirini.
karibuni hata kwa ushauri tu, Qsm ambaye ni mkazi wa Arusha amekuwa ni mmoja tu kati ya jf members sita niliowasajilia ambaye amerudi kwenye hii thread kutoa ushuhuda ,namshukuru kwa kutoa feedback.
Mrejesho zaidi....
Toka nipost kwenye hii thread mara ya mwisho 2013 ,niliendelea kuwasajilia watu waliokuwa wananitafuta baada ya kunisoma hapa hadi hii 2015 nimeendelea, kifupi nimefanya kazi nyingi na watu wa mikoa tofauti tofauti MBEYA,ARUSHA ,KILIMINAJARO,DAR ES SALAAM.LINDI,RUKWA ,PWANI ,SONGEA ,KAHAMA,RUVUMA kwa upande wa limited company na business name, na watu hawa si wote ni member wa jamii forums bali walipata link walivyokuwa wanasearh taarifa za usajili pitia google .Nawashukuruni wote mlioniamini na mnaoendelea kuniamini na kunianganisha na watu wengine, pia itakuwa nzuri zaidi mkija na feedback ktk thread hii ama thread nyingine yoyote mliyopatia taarifa zangu za maswala ya usajili wa company and business names baada ya kupata kazi zenu nilizowasajilia.
pia kuona baadhi ya kazi na feed back ya nilio wafanyia ,waweza pitia thread
https://www.jamiiforums.com/ujasiri...ess-names-na-company-limited-2013-2014-a.html