Msaada juu ya kuuza nyumba ambayo hati ya umiliki bado haijatoka

Sheillah Sheillah

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2020
Posts
653
Reaction score
1,698
Habari.

Nina nyumba ninataka kuiuza. Ila kiwanja kimeshapimwa lakini hati ya umiliki bado haijatoka.

Je, ninaweza kuuza bila ya hati ya umiliki kutoka? Na ni taratibu gani ninatakiwa kuzifuata ikiwa taarifa za upimaji wa ardhi zilichochukuliwa ni zangu?
 
Sina uzoefu sana lkn nadhani kuna mchakato unafanyika, tafuta Mwana sheria nadhani atakusasidia zaidi Ila hata itoke kwa Jina la mnunuzi.
Au fika ofisi ya Aridhi
 
Hiyo itakuwa simple sana nendeni ardhi mkathibitishe kama majina ya mmiliki wa kwanza hajaanza kusoma kwenye systems...

Kama hayajaanza kusoma maana yake mtauziana juu kwa juu halafu mmiliki mpya ataanza harakati za kujisajili upya umiliki.

Ila kama majina ya mmiliki wa awali yanasoma Ardhi watawaelekeza cha kufanya ili mmiliki mpya aweze kubadilisha umiliki...?​
 
Sina uzoefu sana lkn nadhani kuna mchakato unafanyika, tafuta Mwana sheria nadhani atakusasidia zaidi Ila hata itoke kwa Jina la mnunuzi.
Au fika ofisi ya Aridhi
Asante kwa mwongozo mkuu
 
Nahisi yatakywa yanasoma maana walishaniita kuhakiki kila kitu baada ya kupima. Wakaniambia kila kitu tayari nisubiri tu hati ila mwaka na zaidi umepita.

Hapa itabidi niende kweli Ardhi kufuatilia utaratibu itakuwaje. maana nadhani sitaweza kutumia mkataba tu kuuza.
 
mnauziana ila kutakuwa na jukumu la kubadilisha umiliki ambalo nazani muhusika mkuu itakuwa ni huyo mnunuzi...wewe utatakiwa tu kuthibitisha kuwa umemuuzia...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…