Msaada juu ya maana halisi ya neno kimasomaso

oxlade

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2012
Posts
601
Reaction score
96
naomba mwenye ujuzi wa hli neno anipe msaada, maana linanipa utata, nasikia wanawake wakiimba harusini, na wakati mwngne m2 akpendeza huambiwa ametoka kimasomaso.
Mwngne akaniambia kimasomaso ni mtu mwenye jicho la husda ambaye anaweza akaitazama mboga mpaka ikachacha, ndo mana huwa wanaimba kimasomaso mwanangu usimuone.
Je nini maana halisi na sahihi ya KIMASOMASO?
 
Je nini maana halisi na sahihi ya KIMASOMASO?

oxlade . Safari_ni_Safari


Kimasomaso
nm [ki-/vi-] = pretence / pretext:

Kufanya
kimasomaso = to try to get out of a difficult argument, tight corner by trickery e.g. by pretending not to understand or to have forgotten.

==
Swahili Proverbs: Methali za Kiswahili

Kimasomaso mwanangu usimwone. = My son, don't encounter a jealous person.

Kimasomaso, a person who is envious

=====

Fanya kimasomaso in English

Translations into English:

  • be evasive
  • make excuses
  • pretend (verb, adjv )

Kimasomaso:

  • dissimulation (noun)
  • evasion (noun)
  • excuse (noun,verb)
  • hypocrisy (noun)
  • pretence (noun)
  • pretext (noun)

===
 

Heshma kwako mkuu, nimeelewa somo vilivyo.
 
Aisee!!! Kumbe kiswahili ni kigumu namna hii!?
 
Kiswahili ni kigumu kala zilivyo lugha nyinginezo duniani. Ni jambo la kawaida kuwa, hawa wazawa wa lugha wanaweza wasijue kila kitu katika lugha yao. Sio dhambi...kwa hiyo ndio maana watu wanajifunza na kusomea taaluma ya lugha ili wawe wataalamu au wawe na ujuzi.
Kwa hiyo, neno hilo linategemea linatumika wapi - muktadha wa matumizi yake. Ni kama wajumbe walivyoelezea hapo juu.
1) Kimasomaso mwanangu msimuone....wenye mamcho ya husda wasije kumfanyia ubaya nk
2) Ametoka kimasomaso - amewatoa aibu / ameshinda/ nk
Kwa hiyo muktadha ndio unamaanisha matumizi sahihi ya neno.
Kumbuka kuwa LUGHA NI SAUTI ZA NASIBU ZINAZOWAWEZESHA WATU KUWASILIANA. YAANI NI SAUTI ZA KUZUKA TU AMBAZO ZINAWAWEZESHA WENYE LUGHA KUWASILIANA NA KUELEWANA. MFANO 'KIMASOMASO' KAMA AMBAVYO INATUMIKA KATIKA JAMII YETU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…