Msaada juu ya rejesho la jumla la mkopo benki X kuzidi makato

Nashukuru kwa muda wako juu ya Jambo langu, hayo uliyataja nayajua yote, hesabu rahisi mfano umekopeshwa laki 1, utakatwa magarama ya bima na huduma ya mkopo Kama sh 9000/-,utalipwa kwa muda wa miezi 12 na Kila mwezi nilipe 10000/-, hivyo jumla ya hela yao ni 120000/-. Sasa unaambiwa uingize mkopo wa sh 125000/- kwa afisa utumishi.

Hivyo Basi, Kama Kila mwz ni 10000 nilipe kwa miez 12 nitalipa 120000/-. Hii sh 5000/- imetoka wapi? Kwani sikuiona wakati nasaini mkataba wa 120000/-?
 
Ian hoja ya msingi fuatilia
 

Habari,

Ninaweza kukusaidia kufanya mahesabu ila kama utaweza kunipa maelelzo ya kutosha.Nipe vitu vifuatavyo
1. Kiasi cha mkopo
2.riba ya mwezi au mwaka.Pia unatakiwa kuwauliza kama hii ni fixed au floating rate
3.Kiwango amabcho unaweza kurudisha kila mwezi.Hii sio lazima ila itakusaidia sana kufanya mipango namna ya kupunguza ukali wa riba

Asante.
 
Mkopo ni sh 8000000/- na riba ni asilimia 16 kwa mwaka x miaka 8.
Kwa mchanganuo uliotoa kama rib ya 16% iko sahihi ulitakiwa kukatwa TZS 148,230.29 kila mwezi ambayo ni sawa na jumla ya TZS 13,110.051.56 kwa miaka 8 ambapo TZS 5,110,051.56 ni Jumla ya Riba kwa kipindi hicho. Kwa makato ya TZS 138,000 kwa mwezi hayaendani na riba ya 16%. Unless mkopo wako ni chini ya 16% (possibly 13.0% - 13.7 kwa mwaka + Nyongeza za gharama za mkopo na hivyo kupelekea makato ya TZS 138,000/- kwa mwezi). Otherwise urudi benki uliyokopa kwa ufafanuzi zaidi.
 
Ngoja nipitie kipengele kimoja kwa kingine nitakurejerea!
 
Ukiambiwa riba Ni reducing,
Maana ake kinachopungua Ni PESA YA RIBA kadri unavyolipa.

Na Sio pesa ya REJESHO.

Ndo maana unapotop up, unapata Ela kidogo Sana maana pesa nyingi inaelekezwa Kulipa riba
 
Pi
Ukiambiwa riba Ni reducing,
Maana ake kinachopungua Ni PESA YA RIBA kadri unavyolipa.

Na Sio pesa ya REJESHO.

Ndo maana unapotop up, unapata Ela kidogo Sana maana pesa nyingi inaelekezwa Kulipa riba
Pia natambua Hilo!
 
Umesema vizuri.

Loan officers wengi huficha baadhi y taarifa muhimu

Mfano ukikopa mil. 20 Benki utakachopokea ni Milioni 18. Ila utalipa Milioni 20 yote kmaa principal sum na Riba yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…