Msaada Juu ya ufugaji wa Kuku

Msaada Juu ya ufugaji wa Kuku

Dionize N

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
1,848
Reaction score
3,293
Habari zamchana wana bodi, samahani wakuu kwa wale wataalam wa ufugaji wa kuku nahitaji msaada wenu.

Nimeanza kufuga sasa nina mwezi wa tatu. Nafuga kuku chotara wa mayai, nimekumbana na hiki kitu sikielewi kuku wangu wana nyonyoka manyoya migongoni na wanadonoana sana.

Nimejaribu kuwapa vitamins lakini bado tatizo linaendelea. Mdau mwingine akaniambia wanakosa calcium lakini chakula chao kinachanganywa na calcium ya kutosha pia naombeni msaada wenu juu ya hili.

Natanguliza shukran zangu za dhati.
 
Kama umewawekea taa, jaribu kuzima taa mida ya usiku afu uone kama bado wana donoana.
 
Na tabia ya kudonoana wanayo wakati wa mchana na akidonolewa mmoja usipowahi basi wanamuua kabisa maana hawataki kuona kidonda/damu
 
Asubuhi kabla ya kuwapa pumba wape mchicha kwa wingi au chokaa ya kutosha bila ya kuchanganya na pumba Kisha wape pumba baada ya siku 2 au 3 utaona mabadiliko
 
Habari zamchana wana bodi, samahani wakuu kwa wale wataalam wa ufugaji wa kuku nahitaji msaada wenu.

Nimeanza kufuga sasa nina mwezi wa tatu. Nafuga kuku chotara wa mayai, nimekumbana na hiki kitu sikielewi kuku wangu wana nyonyoka manyoya migongoni na wanadonoana sana.

Nimejaribu kuwapa vitamins lakini bado tatizo linaendelea. Mdau mwingine akaniambia wanakosa calcium lakini chakula chao kinachanganywa na calcium ya kutosha pia naombeni msaada wenu juu ya hili.

Natanguliza shukran zangu za dhati.
Jaribu kupunguza mwanga bandani mkuu
 
Jaribu kununua au Kama unaweza kupata damu ya ng'ombe au Mbuzi, kondoo ikaushwe then wape kuku japo chokaa ni dawa pia
 
wanahitaji madini. wengi wameteja baadhi ya madini wamesahau chumvi. waweke kwenye eneo la kutosha. punguza msongamano kama haitasaidia pengine wapo mchanganyiko wa aina mbali mbali utagundua aina moja inaonewa zaidi watenge. pia wakate au wachome midomo itasaidia. lila la kheri mkuu
 
kama utakosa majani mabich kama ulivyoshauriwa hapo juu tafuta vitamini plain kwa ajili ya kuku wa mayai. unaweza kushauriwa vizuri zaidi na mtoa huduma wa duka la dawa za mifugo
 
Na tabia ya kudonoana wanayo wakati wa mchana na akidonolewa mmoja usipowahi basi wanamuua kabisa maana hawataki kuona kidonda/damu
Mkuu tafuta chakula cha Silverland ni kizuri sana huji kuona hiyo kitu ya kudonoana kabisa kama uliko hakipatikani tuwasiliane nikupe namba ya mhusika ili muwasiliane, ningeweka hapa ila sijapata ruhusa yake
 
Kwanza kabisa unatakiwa kuhakikisha kuku wako wana eneo la kutosha ( nafasi katika banda lao) ili wasibanane, kama hilo limezingatiwa ndo uanze kufuata ushauri mwingine uliopewa na wadau wengine hapo juu ikiwemo kuwapa mboga za majani, chokaa, vitamini na chumvi
 
Kwa ushauri wangu nisingekushauri uwazoeshe kuwapa damu kama mdau mmoja alivyochangia hapo juu kwasababu siku ukija kuikosa kuku watakusumbua sana.
 
wape DCP au hypermineral mkuu kwa first aid baadae ndo utaelewa cha kufanya make hawa kuku wanasumbua wakianza huo mchezo
 
Back
Top Bottom