Msaada: Juu ya Ufundi Cherehani anisaidie

Msaada: Juu ya Ufundi Cherehani anisaidie

shinji

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2013
Posts
257
Reaction score
174
Habari,

Nahitaji kujua kushona aina mbalimbali za mavazi.

Je, ni njia ipi bora ya kujifunza kwa mtu au kwenye chuo cha tailoring? Na please kwa anaefahamu kuhusu vyuo bora vya mafunzo hayo naomba anisaidie kwa kuzingatia gharama, muda wa mafunzo na mambo mengine ya kitaaluma hususani kipindi gani mafunzo huanza

Asanteni.
 
Pole, ungeuliza masomo ya chuo kikuu hata asiyejua angejifanya anajua......

Ngoja nijaribu;
> Kujifunzia chuoni ni bora zaidi na mara nyingi huwa ni miezi mitatu na sana sana wengi gharama huwa ni sh. 150,000/= na hiyo huwa ni awamu ya kwanza ambapo wanafundishwa mambo mepesi mepesi na awamu nyingine kukamilisha miezi 6 ndo wanasoma hadi suti.
Vyuo vizuri, jaribu vituo vya MISSION (Vya kanisa hasa RC)

Nadhani nimejaribu
 
Nenda VETA, pia mtafute fundi anayeshona vizuri uwe unajifunza kwake kwa vitendo (huku mtaani unalipia tsh 10000-15000 kwa mwezi). Hakikisha unayo cherehani yako tayari
 
Back
Top Bottom