Msaada juu ya ugonjwa huu ngozi

Msaada juu ya ugonjwa huu ngozi

Bugududu Sududu

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2014
Posts
594
Reaction score
691
Habari zenu wakuu,samahani mi ninasumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa ngozi takribani miaka 4,nimekuwa nikitokewa na vipele ambavyo huanza vikiwa vidogo na laini ukiviminya vinatoa majimaji mfano wa mafuta kadri vinavyokuwa huwa vigumu ukiviminya vinatoka vitu vyeupe katika mfano kama itokavyo dawa ya meno.

Vipele hivi vimetokea sehemu za shingo,kifuani na kwenye makwapa hospitali nimepima baadhi ya vipimo kama;RPR,FTA,VDRL,RFT na Blood culture na majibu yanasema hakuna tatizo,madaktari wamekuwa wakisema labda ni Allergy,Eczema au psoriasis.Nimeonana na specialist wa ngozi hapa Bugando kwa maoni yake yeye anasema hii hali niichukulie kama hali ya kudumu.

kwa maneno ya Dokta huyu naona uwezo wake umeishia hapo.Ninaomba msaada wenu kwa ushauri na fikra.Ahsanteni.
 
Pole sana ndugu...
Ngoja wataalamu waje,naamini utapata majibu ya tatizo lako..!
Happy Nyerere Day..!!!
 
Pole sana rafiki,nowdays magonjwa ya ngozi ni mengi hasaaa
 
Back
Top Bottom