Msaada: Kaka yangu anateswa bila ya hatia

PAGAMECO

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2016
Posts
1,206
Reaction score
1,237
Habari za Asubuhi Wakuu Nina Kaka Yangu Ambaye Mpaka Sasa Hivi Ninapoongea Yupo Lupango Bila Makosa kisa ni Mama Mkwe.

Yaani Mchumba yake Ana mtoto Ambaye alizaa kabla Hawajakutana BT Katika Mahusiano Yao mama Mkwe Alimzushia Bro Kuwa Kambaka yule mtoto Yani Mjukuu wake Na Wakaenda Hospital kuhakiki ikaonekana Sio Kweli Ikabidi Wa Mwachie Huru Lakini Bado Yule Mama Bado Anamuwinda kwa Kumtumia Askari wamkamate na Juzi wamemkamata Tena Na Inavyoonekana Mama mkwe Anatumia Nguvu ya Pesa kwa Sababu kesi Hamna Ila Shida Yake ni Kumshikisha Adabu Bro ..

Msaada Wenu Kisheria Ni Nini ! Kifanyike Ili Bro wangu Awe Free Asisumbuliwe Tena Na huyo mama mkwe na Hao Askari ?...!???
 
Kama tatizo ni huyo binti kupitia mama yake basi silaha zote zimo mikononi mwake (broo wako), akiamua kulia sanaaa sawa tu! Akiamua kukimbia sawa tu, akisimama asifanye chochote wamdakue sawa tu.

Haishangazi saaaaana nnzi kufia kidondani.
 

Kila siku huwa nawaonya na nawashauri Wanaume humu JF kuwa usije ukafanya Kosa Kuoa Mwanamke ambaye tayari alishazalishwa huko na Mwanaume mwingine halafu ukajidanganya kuwa mtaishi nae vizuri na sijui atakuwa na Mapenzi ya dhati na Wewe. Kaka yako kayataka mwenyewe hayo kwani kama ni Mademu ambao hawakuwa na Watoto nadhani hapo Mtaani Kwenu walikuwepo wengi tu ila Kaka yako ' akashoboka ' na huyo aliyezaa sasa ' yamemkuta '.
 
Ni sawa Lakini Mwanamke Aliyezaa Naye Ana haki ya Kupendwa na Kuolewa Kama wanawake Wengine Wamependana Ila Tatizo sio Mwanamke Ni Mama Mkwe
 
Sasa lengo la mama mkwe kumshikisha adabu kaka yako ni nini?

Au mama mkwe hataki binti yake aolewe na kaka yako?

Mchumba wa kaka yako ameshindwa kumkanya mama yake kuwa anamvutugia uchumba?
 
Nenda karipoti ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali MKoa wa Dsm ipo jengo la Mafuta House/ Benjamini Mkapa Towers ghorofa 8
 
Sidhani kama hilo onyo lako lina uhusiano wowote na hili tukio, kilichopo hapa nikionacho mie ndio wanachokiona wengi ni hila za mama mkwe zinazosababishwa na mama huyo kukataa mahusiano ya huyo kijana na mwanae wa kike, hata kama huyo Dada asingekua na mtoto basi huyo mama angeweza kumzushia mengine mengi hata ya wizi na kwa bahati mbaya wizi hauthibitishwi hospitalini wala wapi na angefungwa moja kwa moja, kikubwa huyo kijana akitoka jela aachane na huyo mwanamke hiyo sio familia ya kujihusisha nayo
 
Sasa lengo la mama mkwe kumshikisha adabu kaka yako ni nini?

Au mama mkwe hataki binti yake aolewe na kaka yako?

Mchumba wa kaka yako ameshindwa kumkanya mama yake kuwa anamvutugia uchumba?
Mama Mkwe Shida Yake Kubwa Anataka Amchukue Mjukuu wake Kwa Nguvu Kutoka Kwa Mwanae na Mwanae Hataki

Sent from my VFD 301 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…