Msaada: Kaka Yangu Kahukumiwa Miaka 30 Leo

exalioth

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2016
Posts
2,263
Reaction score
3,897
Kwa ufupi kesi ya kaka angu yeye ni machinga, aliuziwa simu na mtu baada ya kuitumia hiyo simu kama wiki mbili alikamatwa

Kosa ile simu aliyonunua iliporwa kwa nguvu kutumia silaha na kupora vitu baadhi ikiwemo pikipiki, na katika sakata hilo walikamatwa watu watatu akiwemo na yeye.

Wakapelekwa polisi kwa upelelezi badae kesi ikaenda Mahakamani wamekaa miezi tisa mmoja wao alitoka wiki mbili zilizopita wakabaki wawili.

Leo ilikuwa siku ya hukumu na imetokea kama nilivyoeleza hapo juu,

Nimeongea na kaka amelia sana anasema wamefungwa kwa kukosa hela ambapo mwenzao kesi ya pamoja ametoka kwa kutumia pesa. Kwa upande wetu pesa hatuna familia ya kimasikini

Naomba msaada kama kuna utaratibu upi tuutumie kama familia, imeniuma sana kuona kaka anafungwa miaka yote hiyo.

yuda exalioth
Jamiiforms
geita
 
Pole sana ndugu

Ila nina swali kwamba aliemuuzia simu na yupo ndani au ndo huyo katoka?

Na je kaka yako aliuziwa simu akijua ni simu ya wizi?
 
Rahisi ni ghali. Ndicho kilichomtokea kaka yako.

Huko huko GEREZANI kuna askari magereza ambao shughuli zao ni kusaidia wafungwa kukata rufaa. Hivyo na wewe mshauri aongee na askari hao wa kitengo cha sheria akate rufaa mahakama kuu.
 
Simu huwa zinanunuliwa madukani, iweje yeye anunue kwa mtu mitaani? Pili miaka 30 kwa simu tu haiingii akilini, lazima kuna makosa mengine kama ya ujambazi au wizi huyo kaka yako kayafanya. Refer kifungo cha Sabaya kwa miaka kama hiyo.
 
Hizo ni story za upande mmoja unataka kutochota tukuonee huruma.
Ukute yeye ndiye jambaz wanaotembea na boda boda na panga usiku wakikukuta wanakuibia kibabe.
Binafsi sina huruma na mwizi wala mnunuaji wa Mali ya wizi
 
Simu huwa zinanunuliwa madukani, iweje yeye anunue kwa mtu mitaani? Pili miaka 30 kwa simu tu haiingii akilini, lazima kuna makosa mengine kama ya ujambazi au wizi huyo kaka yako kayafanya. Refer kifungo cha Sabaya kwa miaka kama hiyo.
Hyo ni kesi ya robbery ndo mana imekuwa 30

Sent from my TECNO LC6a using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…