Msaada: Kaka Yangu Kahukumiwa Miaka 30 Leo

Msaada: Kaka Yangu Kahukumiwa Miaka 30 Leo

Jamani naomba kuuliza!
Ni simu tu ndio sio vizuri kununua kwa mtu au hata bidhaa za ndani kaama radio, vitanda, fridge nk
Naombeni ufafanuzi kijana wenu nisije kwenda Jera Mana naogopa saana
Vitu vyote ulivyovitaja vinaweza kukufunga miaka dahari na ndio kilichomtokea kaka yangu kuuziwa simu ya kuporwa
 
Kuna sehemu unieleweshe kaka amelia sana kwamba mwenzao alitoka kwa sababu ya pesa sasa kwenye huo uvamizi walikuwa wote na kaka au
Maana umeanza kuwa kaka aliuziwa simu ya wizi na ilitumika silaha katika uvamizi pikipiki na vitu vingine viliporwa sasa hao watatu kuwepo kwenye hiyo kesi nao waliuziwa baadhi ya vitu au?
Aliewauzia aliwakuta kijiweni ambaye yeye ni mskaji wanamuonaga kitaa tu alikua na simu mbili Samsang kaka akanunua moja namwingine ambae yuponae gerezani alinunua simu nyngine mmoja alinunua laptop

walikamatwa watu watatu wawili simu mmoja laptop rakni wiki moja iliyopita wa laptop ameachiwa huru sasa sjui kwanini yeye kaachiwa wakati kesi fail moja
 
Kama ni kweli Tumia siasa kupitia mitandao ya kijamii utengeneze attention. Watatokea wanasiasa kukusaidia ili kupata mtaji wa kisiasa. Mitandao ina nguvu sana, kama kuna kamchezo kalifanyika akaonewa wahusika wakiona mitandao inasema wataanza kutafuta namna kabla wanasiasa hawajalifanyia kazi.
Asante
 
KESI YOYOTE NI HELA japo sio zote.
Wameshindwa kumtoa kituoni.kuendesha rufaa wataweza?
Kuna rufaa mkuu, usimkatishe tamaa... Awatafute akina Tito Magoti kule Twitter wanaweza kumuelekeza kile kituo cha sheria...
 
Kama kweli hii story yake ni ya kweli. Shaenda magereza, kila mtu anasema kaonewa wote hawajakosa, nawaambieni mahakimu we go 98% hawafungi mtu kwa kumuonea
100% Hakimu au Jaji hawamuonei mtu, ni kwamba mtu anafungwa kwa kukutwa na hatia. Sasa amekutwaje na hatia ni swala la namna alivyojitetea dhidi ya ushahidi ulioletwa na Jamhuri.
 
Asante mkuu kwa ufafanuzi mzuri maana kaka hakua na risti yoyote waliuziana kienyeji afu shahidi upande wa pili walikua ni askari waliowakamata
Pole sana ndugu watu wengi sana wanapata shida na kuhukumiwa kwa makosa yasiyo yao kwa kukosa ushahidi wa kujinasua.

Labda hapo angekuwa na watu wa kuthibitisha siku na saa ya tukio alikuwa wapi.

Ni changamoto kwa hii kesi. Fuatilieni hukumu mpate mwenendo wake muone mapungufu hapo mnaweza kukata rufaa.
 
Ni sawa lakini kwa nchi zetu hizi, masikini anaonewa sana, kwenye upatikanaji wa haki yake, juzi kuna jamaa , ameachiwa huru baada ya kukaa jela miaka 34, kwa kosa la mauaji, ambalo jaji aliyemuhukumu alimwambia ushahidi haujitosherezi, wa kukufunga ila kutokana na usalama wako, nakufunga maisha!!hahaaaa!!!badaye jaji mwingine alipoipitia akashangazwa na hiyo hukumu, kutokana na ushahidi, na jamaa hata hakukata rufaa!!mwaka jana anashangaa tu anaachiwa!!!
Too good to be true.

Hii ni stori ya kijiweni haina ukweli wowote. Kazi ya usalama wa raia siyo ya mahakama. Mahakama ni chombo cha kutoa haki. Inachoweza kuamuru ni huyo mwananchi kupewa ulinzi na sio kifungo cha maisha.

Huo ni uongo.
 
Jamani naomba kuuliza!
Ni simu tu ndio sio vizuri kununua kwa mtu au hata bidhaa za ndani kaama radio, vitanda, fridge nk
Naombeni ufafanuzi kijana wenu nisije kwenda Jera Mana naogopa saana
Jitahidi kuwa na ushahidi wa manunuzi ikibidi hata serikali ya mtaa.
 
Hatari sana,ilishawahi kumtokea jamaa yangu,yeye alikuwa konda wa daladala,zile zinapiga kazi usiku kuanzia saa 4 mpk asubuhi,nadhani mtakuwa mnazijuaJamaa yule asubuhi wakati anafagia gari akakuta kuna simu ya Iphone iko safi,alichofanya akabadilisha line akampeleka mkewe,kumbe ile simu iliibwa sehemu ule usiku na mali nyingine,wale wezi walisafiri na ile daladala mmoja wao alidondosha ile simu,maana kwa maelezo yake ni kuwa kuna mmoja wa wasafiri alilala siti ya nyuma kabisa.Basi mwenye mali aliripoti Polisi wakaanza kuitrack mpaka wakamkamata mkewe,jamaa akapata habari alipokuja kituo cha polisi wakamdaka kwa kosa la wizi wa kufanya uhalifu na kuiba.Bahati yake mwenye simu alichohitaji ni simu yake tu ndio ilikuwa cha muhimu kwake,sasa mbinde ilikuwa ni polisi kumuachilia jamaa,kifupi ni kuwa ilibidi tuzame mifukoni wakamuachia...
 
mmmh hatari
 
Amuachie Mungu?
Una akili timamu jombaa?
😄
Hivi huyo jamas sikumwelewa maana Mungu katupstia kila kitu. Sa sijui anatakaje kumwachis Mungu. Apambane na aombe Mungu ampe njia.
 
Too good to be true.

Hii ni stori ya kijiweni haina ukweli wowote. Kazi ya usalama wa raia siyo ya mahakama. Mahakama ni chombo cha kutoa haki. Inachoweza kuamuru ni huyo mwananchi kupewa ulinzi na sio kifungo cha maisha.

Huo ni uongo.
Mkuu tena usiseme kitu kabisa!!kwenye mahakama zetu hizi, kidogo kwa sasa afadhari , hapa tunazungumzia kesi ya mwaka ya 1987!!na watu walipigania sana haki ya kijana, lakini wapi?kama siku ya kumzika huyo rafiki yake aliyeuawa na majambazi , huyo mtuhumiwa alishirikiana na wana ndugu tangu akiwa icu, hadi akafariki, baada ya wiki 3 ndio anafuatwa na kuambiwa alihusika,
 
Kwa ufupi kesi ya kaka angu yeye ni machinga, aliuziwa simu na mtu baada ya kuitumia hiyo simu kama wiki mbili alikamatwa

Kosa ile simu aliyonunua iliporwa kwa nguvu kutumia silaha na kupora vitu baadhi ikiwemo pikipiki, na katika sakata hilo walikamatwa watu watatu akiwemo na yeye.

Wakapelekwa polisi kwa upelelezi badae kesi ikaenda Mahakamani wamekaa miezi tisa mmoja wao alitoka wiki mbili zilizopita wakabaki wawili.

Leo ilikuwa siku ya hukumu na imetokea kama nilivyoeleza hapo juu,

Nimeongea na kaka amelia sana anasema wamefungwa kwa kukosa hela ambapo mwenzao kesi ya pamoja ametoka kwa kutumia pesa. Kwa upande wetu pesa hatuna familia ya kimasikini

Naomba msaada kama kuna utaratibu upi tuutumie kama familia, imeniuma sana kuona kaka anafungwa miaka yote hiyo.

yuda exalioth
Jamiiforms
geita
Nenda kwenye legal human right center watakusaidia bure kukata rufaa
 
Back
Top Bottom