Msaada: Kaka yangu kichaa, alivuta bangi sana zamani

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Wakuu.

Kaka yangu ni kichaa fulani, alikula msuba(bangi) nyingi sana zamani,mm nikiwa mdogo ,bila kazi ya kipato.

Kaka yangu ni nguzo ya Taifa na ni msaada mkubwa sana.

Nifanyeje kumtibu?Kama kuna dawa au chochote naomba niambiwe. Siwezi kumwacha kaka.

Asante.
 
milembe na sober zipo kwa ajili yake chagua kwa kumpeleka

be___blessed
 
Ninakupa Dawa ya kumtibu kaka yako huo ugonjwa wa ukichaa cha bangi fanya hivi Mumfungie chumbani kwa muda wa siku 3 kwa siku ya kwanza apatikane mtu wa kumpiga mikanda mwilini asubuhi kwa muda wa dakika 10 amtandike barabara mgonjwa kisha mumpe chakula ale. Chakula chenyewe wali apikwe na kuku wenye supu ya pilpili mtama na tangawizi. Na Wakati wa jioni apigwe tena mikanda kwa muda wa dakika 10 kisha aogeshwe na kama ana manywele mengi kichwani akatwe na aogeshwe na kupewa chakula kama mulivyo mpa asubuhi. Apigwe kwa njia hizo kwa muda wa siku 3 ila wakati wa mchana munaweza kumpa chakula pasipo na kumpiga .Baada ya siku 3 mumchukuwe kaka yako mgonjwa mumpeleke Karibu na makaburini usiku iwe saa 6 usiku mumfunge kitambaa cheupe usoni mumpeleke kwenye kaburi lolote akae kwenye hilo kaburi mumu ambie ahesabu moja mpaka 100 anapo anza kuhesabu muondoke hapo mumu ache peke yake atakapo maliza kuhesabu na kufunguwa kitambaa usoni atajiona yupo makaburini ataondoka kurudi nyumbani. Akifika nyumbani asiingie chumbani au chumba chochote mumpeleke chooni akaoge kwa maji ya chumvi ya mawe , na kuziacha huko huko chooni nguo zake alizo toka nazo makaburini mumpe nguo mpya zile nguo zake mukazitupe atakuwa amekwisha kupona. Jaribu utakuja kunipe Feedback.
 


binafsi nimecheka jaman
 
Bangi isihusishwe kwenye mambo ya kijinga...

Ndugu yenu ndiyo kamfanya kuwa ndondocha
 
ushirikina on work.
 
duuuuuh

be___blessed
 


Inaonekana huyo alikatazwa kutumia bangi ila alikaidi kwani kile ni kilevi/dawa iliyolaaniwa....pole zake.
 
[emoji2] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] aiseeee! Nimecheka sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kaka yako sio bangi iliompa huo ukichaa bali kwenu nasikia mnaugonjwa wa kichaa wa asili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…