PENYE MITI KWELI HAPANA WAJENZI,
Swali la Pauline la mnaishije? ni zito sana,kupitia jibu lako unaweza kupata,
kwa nini huyo mkeo anaanza jeuri ktk kipindi kifupi sana cha ndoa yenu,
pia swali la nyumba kubwa, je uelewa wake ukoje?,nalo ni muhimu sana
Isiwe ni aina ya mwanamke anayechukulia kupendwa kama silaha ya kumnyanyasa mwanaume.
Usitafute nyumba ndogo, bali ongea naye pamoja na watu wenu wa karibu mnaowaheshimu, asipokuelewa mpe muda akapumzike kwao kidogo akiwa huko kama hana mpenzi wa pembeni basi atajirekebisha.
KILA jambo likizidi lina ubaya wake Yawezekana upole wako umezidi kipimo, so yeye anauchukulia ndivyo sivyo kabisa.
Natamani kama ungekuwa wangu.....lol
HONGERA SANA UAMINIFU WAKO,NA ENDELEA KUWA MWAMINIFU NA KUIHESHIMU NDOA YENU, NAAMINI HILO NI WIMBI TU LA KUPITA KUWENI MAKINI,
LISIJEZAMISHA NDOA YENU. POLE SANA, USIPATE PRESSURE ILA HAKIKISHA UNALIPATIA UFUMBUZI HARAKA.