Habari wana JF wenzangu,
Kwanza samahani kwa kutumia jukwaa ambalo sio sahihi lakini naona litanisaidia zaidi maana watembeleaji wake ni wengi.
Naomba msaada nimekuwa na tatizo la kutokwa na damu sehemu ya haja kubwa ( Unyeo/ ------) kila ninapoenda kujisaidia ila hapaumi wala nini..!! Nimeenda hospital Burhan na Hindu Mandal wakanipa dawa ya tube ambayo ni cream kwa ajili ya kuingiza sehemu husika mara 3 kwa siku, lakini naona tatizo haliishi. Plz naomba msaada maana linanichanganya sana jamani.
Nawasilisha.
Pole sana kwa hilo tatizo, labda nikuulize swali moja, je kuna uvimbe wowote mdogo ambao umejitokeza na kuning'inia kidogo nje ya hayo maeneo? Kama ni ndiyo inaweza kuwa Piles/hemorrhoids. Hivi ni vivimbe ambavyo hutokea njia ya haja kubwa na kwa wengine huleata maumivu na kwa wengine inaweza isilete maumivu. Unaweza kwenda Agha Khan kumuona Dr. Athenary (sijui kama jina nimelipatia) au surgeon yeyote anaweza kukusaidia.
Kama hakuna uvimbe wowote inaweza kuwa ni rectal bleeding ambayo husababishwa na mambo yafuatayo:
Anal cancer
Anal fissure (tear in the skin of the anus)
Angiodysplasia (abnormalities in the blood vessels near the intestines)
Colon cancer
Colon polyps
Constipation
Crohn's disease
Diarrhea
Diverticulosis (a bulging pouch that forms on the wall of the intestine)
Food poisoning
Hemorrhoids - hii niliitaja hapo juu
Intussusception (a portion of the intestine slides inside another portion)
Ischemic colitis (colon inflammation caused by reduced blood flow)
Proctitis (inflammation of the rectum)
Pseudomembranous colitis (colon inflammation caused by an infection)
Radiation therapy
Rectal prolapse (part of the rectum protrudes through the anus)
Solitary rectal ulcer syndrome (a sore on the wall of the rectum)
Ulcerative colitis
Hapo Aga Khan au Muhimbili wanaweza kukusaidia kukupa uchunguzi wa haraka. Jitahidi uende mapema kabla tatizo halijawa kubwa.
Pole na kila kheri,
HP