Msaada katika kesi ya mahusiano

mahirtwahir

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2013
Posts
613
Reaction score
313
Habari waungwana.

Niko na mjomba wangu ana umri wa miaka 17 wa kiume kajenga mahusiano na msichana alie na umri sawa na huo maana wako darasa moja.

Jana jioni mtoto wa kike alikamatwa na barua iliotoka kwa mwanume ambaye ndio huyo mjomba wangu ya mahaba nadhani wengi wenu mutakumbuka mapenzi ya shule yalivyo mawasiliano ni barua.

Baaada ya kuonekana na barua wazeee wake wakamgombeza na kumpiga huku wakimuambia kua kuna simu ilipotea inaonekana yeye ndio kaiba binti alikubali kweli na kusema kua amempa huyo mjomba wangu kisha binti katoroka kwao toka jana hadi sasa hajarudi na hivi sasa wazee wameamua kutoa taarifa polisi na ikabidi aitwe dada angu na mwanawe waende kituoni kwa mahojiano.

Mtoto wa kiume alipoulizwa kua jeee kapewa simu na huyo bint anasema nikweli alipewa na ameshaiuza kitambo?

Jeee hapa sheria inakuwaje kwa huyu mwanaume na jeee utetezi wake utakuaje?
 
Duuu kaka lakini mwanaume hujui aliambiwaje anaweza kuambiwa kua ameiokota kwa hio wizi ni wa bint ama mwanaume
Acssory after the fact
Hapo ni kwamba anatuhumiwa kwa wizi wa simu
Pia kutokujua sheria c kinga mkuu
 
Hao hawajafikisha umri wa miaka 18 hivyo upande wao wote wako right.Lakini hapo mwizi ni ke na siyo me.Atalipa simu tu basi hiyo si ni kesi ya wizi au imefunguliwaje mahakamani.
 
Hao hawajafikisha umri wa miaka 18 hivyo upande wao wote wako right.Lakini hapo mwizi ni ke na siyo me.Atalipa simu tu basi hiyo si ni kesi ya wizi au imefunguliwaje mahakamani.
Bado haijafunguliwa ila mama wa mwanaume na mwanawe wameitwa polisi kwa mahojiano
 
Huo ni wizi nashauri mlipe hiyo simu na myamalize nje ya vyombo vya sheria ni mimi Wakili msomi Funzadume
 

JITAHIDINI MUIVUTE KESI NJE DOGO ATAINGIA KWENYE SHIDA
 
Huyo mpwa wako ni boya. Anauza simu ambayo ingemsaidia kuchat na kufikisha ujumbe sasa anaandika barua ambazo zinaishia kufumwa!
 
Hao wote ni wezi huyo kijana alipoletewa simu hata kama aliambiwa imeokotwa angetakiwa akushirikishe wewe mlez wake yeye kauza alafu pesa kapeleka wapi istoshe wewe kila siku unampa pesa ya shule huyo usipokua nae makini anaelekea kubaya anaweza kuiba hata vitu vidogo nyumbani bila wewe kujua' usishangae ukaambiwa ndie alimshawishi bint akaibe' Tafakari sana mkuu watoto ndivyo wanaazaga hivyo baadae usijejuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…