Msaada katika ndoa: Mwaka wa tatu kwenye ndoa sijapata ujauzito

kengeledoi

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Posts
325
Reaction score
230
Habari wakuu, natumaini mpo poa. mimi nimeolewa huu mwaka wa 3 ila sijabahatika kupata mimba na siku zangu huwa nazipata vizuri na hata siku za hatari nakutana na Mr. ila sijafanikwa.
Naomba mnisaidie au sijui kuhesabu siku zangu vizuri.
 
Enda Suphai?...Sababu zinaweza kuwa nyingi mno moja wapo ikiwa ni huenda si wewe mwenye shida bali ni Mume wako hana uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito so ni vema muende kwa wataalam wa masuala ya uzazi kwa check-up....Lakini kama uko na mzunguko wa siku 28...Hesabau siku nne za hedhi plus siku 7 za salama hapo huwezi pata ujauzito..Jumla inakuwa siku 11...So kuanzia siku ya 12-13 hapa ukikutana na baba totoo unauwezo wa kupata mtoto wa kike na siku ya 14-16 hapa ukikutana na baba totoo utapata ujauzito pia na kuna uwezekano mkubwa wa kupata mtoto wa kiume....So kuanzia siku ya 17 mpaka uje upate hedhi hizo ni siku salama...huwezi pata ujauzito...Hii ni kutokana na experience yangu na imenisaidia kupata mtoto wa kike na wa kiume kwa kufuata utaratibu huu..
 
Habari kiongozi, aksante kwa ufafanuzi mzuri,
Je kwa mama mwenye mzunguko wa siku therethini (30) inakwendaje?
 
pole ila kumbuka watoto ni baraka kutoka kwa MUngu muda ukifika utapata ila kama una wasi wasi nenda kacheki afya ya kizazi anza kwenda wewe kwanza ukiwa safi mwambie mwenzio muende wote. nia ya kukwambia uende kwanza wewe ni kuwa na uhakika kuwa wewe huna tatizo maana mijitu mingine migumu kelewa unaweza ukawa na tatizo akijua akaanza kutumia uzaifu wako kukunyanyasa...
 
Habari wakuu, natumaini mpo poa. mimi nimeolewa huu mwaka wa 3 ila sijabahatika kupata mimba na siku zangu huwa nazipata vizuri na hata siku za hatari nakutana na Mr. ila sijafanikwa.
Naomba mnisaidie au sijui kuhesabu siku zangu vizuri.

Ni Pm nikusaidie
 

Asante mkuu, vipimo nimeshafanya na kimebaki kimoja nafanya next week will come to update you the status ila Mr. ndo bado hajakamilisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…