Msaada: Kibali cha biashara - Arusha

Kaka Joni

Member
Joined
Oct 1, 2013
Posts
25
Reaction score
16
Wadau,
Katika kujikwamua na hali mbaya ya kiuchumi, nimehamua kufungua biashara jijini Arusha eneo la sanawari. Tatizo ni kwamba eneo nililopata liko kwenye makazi ya watu. Nimeongea na balozi ananiambia kuna vikao inabidi vikae sijui kujadili na milolongo mingine mingi tuu na kwamba inabidi nionane na watu chungu nzima.. Sasa mimi sio mkazi wa Arusha huwa nakuja tu na kuondoka na muda wangu nimchache.
Wakuu, naomba kama kuna mtu anaefahamu ni nani naweza "kumuona" hapa Arusha ili nipate msaada wa kuweza kupata vibali na vitu vingine ili nianze biashara mara moja! Ntashukuru sana
 

Ni biashara gani?
Hilo ndio la Muhimu kuliko Balozi.
 
Hiyo lazima itakuwa ni bar ndo mara nyingi ukataliwa kwenye makazi ya watu,.. KAKA JONI sema ni biashara gani maana mimi nipo Arusha pIA,..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…