MSAADA:kibari cha kubadilishana kituo cha kazi

MSAADA:kibari cha kubadilishana kituo cha kazi

Brbm

Member
Joined
Apr 16, 2014
Posts
71
Reaction score
6
Jamani mi nataka kujua eti mtu unapokuwa umeshasainisha barua zako za kubadilishana vituo pande zote kuna kibali unachoandikiwa na Ps wa DED kabla ya kwenda kwa RAS je kile kibali kile unapaswa ukipeleke wapi kwa RAS au unamtumia mwenzako unayebadilishana nae ili kujua kama huku kakubaliwa kuna nafasi?
 
Ukisha sainisha kote[kwako na kule unapokwenda] unachukua kibali cha kukubaliwa kule unakotaka kuhamia then unarudi kwa afisa utumishi wako atakuandikia covering later ambayo utaipeleka Kwa RAS mwenyewe bt sharti uwe na 1 Barua yako ya kuomba uhamisho, copy ya kitambulisho chako, 3 salary slip copy ya ivi karibuni, na barua ya kuthibitishwa kazini kama umeshapata. NB NI NZURI UIPELEKE MWENYEWE NA MAPEMA ILI KAMA KUNA MAPUNGUFU WAKWAMBIE UYAREKEBISHE.
 
Jamani mi nataka kujua eti mtu unapokuwa umeshasainisha barua zako za kubadilishana vituo pande zote kuna kibali unachoandikiwa na Ps wa DED kabla ya kwenda kwa RAS je kile kibali kile unapaswa ukipeleke wapi kwa RAS au unamtumia mwenzako unayebadilishana nae ili kujua kama huku kakubaliwa kuna nafasi?

Mwalim, kitendee haki Kiswahili, umeona heading yako?

Dah. Inasikitisha sana.
 
Barua uliyoomba uhamisho iliyopitishwa sehemu zote, barua ya nafasi kule unakoenda(wanakujibu unakoenda) ,kibali cha uhamisho (atakuandikia ps wa Ded au utumishi), Then kitambulisho cha kazi na current salary slip .vyote hivi utafunga mafungu 3 .moja litabaki masijala wilayani kwako ,mawili utaenda nayo kwa Ras moja atabaki nalo na jingine atatuma tamisemi .
 
Kwahiyo hiyo barua ya kuonesha kule umekubalika ndo ipi? Hebu fafanua
 
Back
Top Bottom