Msaada: Kichwa kujaa maji

Msaada: Kichwa kujaa maji

specialist88

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2014
Posts
1,140
Reaction score
618
Habari wana JF.

Ndugu zangu kuna shida inamsumbua jirani yangu,nimeona niilete hapa jukwaani ili tuone namna yakumsaidia huyu binadamu mwenzetu.

Kuna familia moja (majirani zangu) walipata mtoto wao (first born) wakike-mwaka jana mwanzoni. Kwa bahati mbaya, mtoto wao alizaliwa na tatizo la kuwa na kichwa kikubwa, kichwa kinaongezeka kadri muda unavyoenda. Mtoto amefanyiwa operation, amewekewa mpira wa kutolea maji kichwani lakini wapi! Kichwa bado hakipungui.

Hii familia imehangaika katika hospitali za KCMC, SELIAN na MUHIMBILI lakini wapi! Tatizo bado lipo pale pale! Kibaya zaidi hii ni familia isiyo na kipato kikubwa, mke ni mwalimu na baba ni mfanya biashara ndogo ndogo tu.

Kwakweli, hii familia imehangaika vya kutosha mpaka nawaonea huruma! Kila siku wao ni hospitali. Imefikia hatua mpaka baba mtoto ameacha biashara yake angalau amsaidie mke wake kukaa na mtoto, maana mke wake hawezi kumbeba kumpeleka hospitali kwa jinsi alivyo mzito huyo mtoto, maana kwa sasa tumbo la mtoto nalo limeanza kuwa kubwa.
-----------------------------------

Sasa naomba ndugu zangu, kama kuna mtu/ watu wenye uwezo wa kiushauri, kipesa au mwenye kuweza kum-connect na watu wanaoweza kumsaidia (kama wafadhili, mashirika yanayopelekaga watoto nje au India kufanyiwa matibabu) naomba wajitokeze kuisaidia hii familia tafadhali.

Nawaomba ndugu zangu jamani tuisaidie hii familia.
 
Poleni kwa hilo... huyo mtoto alitakiwa kuwa chini ya uangalizi maalum Muhimbili, ndio kuna kitengo maalumu kwa ajili ya hayo matatizo. Ule mpira hutoa maji kichwani na kuyaleta tumboni, sasa inabidi achekiwe kwa nini na tumboni yasitoke.

Hata maji yakipungua kichani ni ngumu sana kwa kichwa kurudi katika hali ya kawaida kwa sababu hata fuvu la kichwa huwa linakuwa limetanuka. Asihangaike na hospitali nyingine aende Muhimbili tu. Wakati huohuo waendelee kumwomba Mungu.
 
Ningependa kujua imani yao: Nataka niwashauri kitu!
 
Poleni kwa hilo... huyo mtoto alitakiwa kuwa chini ya uangalizi maalum Muhimbili, ndio kuna kitengo maalumu kwa ajili ya hayo matatizo. Ule mpira hutoa maji kichwani na kuyaleta tumboni, sasa inabidi achekiwe kwa nini na tumboni yasitoke.

Hata maji yakipungua kichani ni ngumu sana kwa kichwa kurudi katika hali ya kawaida kwa sababu hata fuvu la kichwa huwa linakuwa limetanuka. Asihangaike na hospitali nyingine aende Muhimbili tu. Wakati huohuo waendelee kumwomba Mungu.

wasa ndugu,nitamshauri arudi tena muhimbili
 
ni wakristo(walokole)

Well, ushauri wangu hauwafai...

Watu wanaumwa kwa sababu tatu:
  • Mabadiliko ya mwili kikemikali yanayosababishwa na mwili wenyewe, vimelea vya magonjwa au vichoheo vya kawaida vya nje, haya huleta magonjwa ya kawaida kama Maleria n.k ambayo hutibiwa kwa dawa na vifaa tiba vya kikemikali, iwe hospitali za magharibi, za kiafrika au za namna nyingine.
  • Mambo ya Kiroho: Kwa kusababishiwa na watu, kukutana na mapepo bahati mbaya na kadhalika na huweza kusababisha madhara ya kikemikali mwilini. Ndio, unaweza kulogwa, kukutana na pepo na ukaumwa ugonjwa wa kawaida kabisa, changamoto yake ni kuwa kupona kwa dawa za kawaida ni changamoto.
  • Kusababishwa na nguvu kuu: Miungu na mizimu huleta magonjwa kama njia ya kuonya, kutahadharisha, kulipa kisasi na wakati mwingine kushinikiza mambo fulani miongoni mwa binadamu.
Kila namna ya kuingia kwa ugonjwa una namna yake ya kutoka na isiyofanana wala kufanya kazi kwenye mazingira tofauti: Ukiumwa Homa ya Plasimodiamu kisha ukaenda kanisani au kwa mganga wa kienyeji unakufa huku unaona, na kinyume chake. Ubaya ni kuwa madakitari wa mrengo mkuu hawakubali kuwa namna zao zimefeli katika mazingira fulani, kila siku wana majibu mapya, matumaini mapya na yote yanafeli, kisha mzunguko ukarudi mwanzo.

Nionacho mimi ni kuwa dogo anaangukia katika makundi mawili ya mwisho, aidha wamemtupia madudu, au ni mambo ya miungu na mizimu. Kutibu kwa namna moja kunafungua njia ya kufahamu cha zaidi kinachomsibu - Nashauri mfanye tambiko kwa mizimu yenu, mtoe sadaka ya upatanisho kwanza: kwa mizimu kuokoka ni kuasi!

Baada ya hapo mnaweza kutoa sadaka zingine kadiri yamaelekezo mtakayopewa na kuhani wa kabila lenu. Huo ni mwanzo na utatoa mwanga mzuri wa kinachomsibu mwanenu.

Mizimu yenu iwape kibali!
 
daaah!speechless
 
Pole sana inasikitisha may be mtumie vyombo vya habari watakaoguswa watachangia. Kingine itisheni harambee kama ninkanisani au wapi ili watu wachangakie. Rafiki ya mtt wangu alikuwa na shida kama hii na mwanae alifanyiwa operation nairobi hospital na sasa yuko sawa ila ilicost milion saba. Namweka kwenye maombi Mungu atafungua njia atapona.
 
Back
Top Bottom