Kichwa Ngumu
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 1,726
- 314
na uzuri wote huo kikojozi!ki ukweli na mimi nilikuwa nikikojoa kitandani.jamani ni aibu,na nilikuwa sifanyi makusudi,unaota una mkojo na uko chooni,mara unaumwaga kitandani.baadae niliacha nilivyofika 14.hakuna dawa yoyote niliyotumia ilitokea tu nikaacha.nina amini baadae ataacha tu.pole yake
Mkuu MziziMkavu,nashukuru kusikia ombi langu na kuja hapa.
Mtoto mwenye ni binti mkubwa, na je hilo kwato la ng'ombe anashika au ananusa? Na vp halitaisha kwa siku 7 au tunakua tunabadilisha?
Natanguliza shukran,
Mkuu Larusai Mux fuata nilivyo kueleza anapanda juu ya mti amevua nguo awepo yeye na mama yake kisha kwato la ng'ombe tia kaa la moto kisha mama yake anampatia hilo kwato la ng'ombe lenye kaa la moto akiwa juu analinusa hilo kwato kisha anakojoa huko huko juu kisha anashuka juu ya mti anavaa nguo zake afanye hivyo hivyo asubuhi na jioni kwato hilo hilo moja kwa muda wa siku 7.Mkuu MziziMkavu,nashukuru kusikia ombi langu na kuja hapa.
Mtoto mwenye ni binti mkubwa, na je hilo kwato la ng'ombe anashika au ananusa? Na vp halitaisha kwa siku 7 au tunakua tunabadilisha?
Natanguliza shukran,
Mkuu Mamndenyi Kwato la ng'ombe ni mguu wa ng'ombe jamani ananunuwa mguu wa ng'ombe anatoa kwato lake la chini kwenye huo mguu wa ng'ombe.Kwato ana maana ni ile ya kutembelea yaani inachomolewa ikiwa nzima nzima wachagga wanaita ni 'mbuachi' kile kigumu cha chini watengeneza makongoro waambie nataka kile cha chini huwa kipo kama kikombe hivi.
Mkuu KIBURUDISHO wha is Mhhh!!!???? Unashangaa nini Mkuu? kashangae baharini Shillingi inazama meli inaelea juu kwa juu.:becky:Mhhh!!!????
Mkuu Mamndenyi Kwato la ng'ombe ni mguu wa ng'ombe jamani ananunuwa mguu wa ng'ombe anatoa kwato lake la chini kwenye huo mguu wa ng'ombe.
Mkuu Larusai Mux fuata nilivyo kueleza anapanda juu ya mti amevua nguo awepo yeye na mama yake kisha kwato la ng'ombe tia kaa la moto kisha mama yake ana
mpatia hilo kwato la ng'ombe lenye kaa la moto akiwa juu analinusa hilo kwato kisha anakojoa huko huko juu kisha anashuka juu ya mti anavaa nguo zake afanye hivyo hivyo asubuhi na jioni kwato hilo hilo moja kwa muda wa siku 7.
Mkuu.@Larusai Mux Hiyo ni dawa haina haja ya kuwa ni bint mkubwa ukubwa wake kama nini tembo? Ana miaka mingapi? kama hataki mpeleke Hospitali basi akatibiwe......Mkuu Mzizimkavu bado nashkuru, yaani uchi bila hata nguo!!!!!!!,binti mkubwa atakubali kweli!
! Ila ntawapa huo ushauri mkuu.
Mimi nimekojoa mpaka miaka 13!! nilichemshiwa ndevu za mahidi ikashindikana, nikaambiwa kunywa maji ya mchele pia haikusaidia.. Bibi mmoja aliniletea majani yale yanayoota kwa kutambaa kwa jina la kiketu mara yanaitwa RUSALAGASI. Ukingoa unakuwa kama mkanda mrefu tu, nikawa navaa wakati wa kwenda kulala asubuhi navua.. kwa muda wa siku 14 tatizo likaisha kabisaa mpaka sasa.
Ushauri wangu ni kumpeleka huyo niece wako kwa daktari afanyiwe uchunguzikamili kuweza kutambua matatizo yake. Kama wakuu wengine walivyochangia katika tatizo hili dawa za ugonjwa huu zinatumika kwa muda mrefu kidogo up to 6 to 12 weeks. Kama ni matatizo ya Misuli ya kibofu cha mkojo (detrusor muscles) anaweza kupewa mchanganyiko wa dawa mbili-imipramine na propantheline.