Msaada kilimo cha chinese

KeyceNjou

Member
Joined
Mar 28, 2014
Posts
9
Reaction score
2
Habari zenu waungwana humu ndani, hope mko njema that y twakutana humu, ombi langu naomba wenye ujuzi ktk kilimo cha mbogambogo wanisaidie maujuzi ya kilimo cha chinese, kuanzia kuandaa shamba hadi mavuno!, imani yangu nitapata somo zuri kama nilivyopata somo la vitunguu swaumu now nipo namalizia kutengeneza matuta nijaribu ! Asanteni,
 
1. Andaka kitalu(Upana 1M na urefu at least 2-4 M), weka mbolea ya samadi
2. Sia mbegu kwenye kitalu (zitakaa kati ya wiki 2-4 ndipo unahamisha(transplanting) kwenye Shamba (main field) ambalo unatakiwa uliandae kabla ama baada ya kusia mbegu kwenye kitalu katika namna hii hapa chini

i. Andaa Shamba, weka mbolea yoyote kati ya ( samadi/ kuku/popo)
ii. Lima, fanya (harrowing), tengeneza vitalu venye upaa wa 1 Mita na urefu inategemeana na maamuzi yako utakovyo iwe
ii. Miche/ seedlings ikishakuwa tayari hamisha kwenye Shamba uliloliandaa panda mche Mmoja mmoja Kwa kila shimo Kwa nafasi(30-45 cm mche Hadi mche na 45- 75 cm mstari Hadi mstari kutengemea na aina/variety ya Chinese cabbage)
iii. Fanya huduma/management za Shamba kama kawaida(mwagilia maji, palizi, kuweka mbolea ya kukuzia kama urea,SA ,kupiga Dawa za wadudu) na utaanza kuvuna Dani ya siku 30-40 baada ya transplanting
 
Nami nimepata kitu. Vipi kuhusu kuweka manyasi/matandazo baada ya kuhamisha miche
 
Nami nimepata kitu. Vipi kuhusu kuweka manyasi/matandazo baada ya kuhamisha miche
Unaweka kama yanapatikana Kwa urahisi au utayapata Kwa gharama ndogo yanasaidia kutunza unyevu kwenye udongo(conserve soil moisture) hivyo hupunguza umwagiaji maji wa mara Kwa mara
Ila kama maji kwenye Shamba lako sio tatizo Haina haja ya kuweka matandazo maana yatakuongezae mzigo wa kazi (workload) tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…