1. Andaka kitalu(Upana 1M na urefu at least 2-4 M), weka mbolea ya samadi
2. Sia mbegu kwenye kitalu (zitakaa kati ya wiki 2-4 ndipo unahamisha(transplanting) kwenye Shamba (main field) ambalo unatakiwa uliandae kabla ama baada ya kusia mbegu kwenye kitalu katika namna hii hapa chini
i. Andaa Shamba, weka mbolea yoyote kati ya ( samadi/ kuku/popo)
ii. Lima, fanya (harrowing), tengeneza vitalu venye upaa wa 1 Mita na urefu inategemeana na maamuzi yako utakovyo iwe
ii. Miche/ seedlings ikishakuwa tayari hamisha kwenye Shamba uliloliandaa panda mche Mmoja mmoja Kwa kila shimo Kwa nafasi(30-45 cm mche Hadi mche na 45- 75 cm mstari Hadi mstari kutengemea na aina/variety ya Chinese cabbage)
iii. Fanya huduma/management za Shamba kama kawaida(mwagilia maji, palizi, kuweka mbelea ya kukuzia kama urea,SA ,kupiga Dawa za wadudu) na utaanza kuvuna Dani ya siku 30-40 baada ya transplanting