Msaada kilimo cha hoho

Habari wakuu naomba tubadilishane mawazo ama tupeane ujuzi wa namna ya kupambana na magonjwa katika pilipili hoho wakati wa msimu wa mvua
Naomba kuwasilisha
 
Mkuu wewe unalimia wapi na wateja wako wako wapi?

Mwezi ujao nataka kuandaa shamba la mboga mboga hekari mbili

Ambalo nataka liwe na mchanganyiko wa mboga zote

Yaani liwe na bamia liwe na hoho liwe na ngogwe(nyanya chungu) hivyo vitu vitatu.
 
Mkuu wewe unalimia wapi na wateja wako wako wapi?

Mwezi ujao nataka kuandaa shamba la mboga mboga hekari mbili

Ambalo nataka liwe na mchanganyiko wa mboga zote

Yaani liwe na bamia liwe na hoho liwe na ngogwe(nyanya chungu) hivyo vitu vitatu.
Mkuu mimi nalimia morogoro wateja wangu ni hapa moro na Dar na Dodoma wew uko wapi
 
Tutembeleane sas huvi mimi niko kwenye kupanda yaani nina transplant kwa uzoefu wangu dar mara nyingi wanaanza kupanda kuanzia miezi ya kt wa 5-6
Okey sasa mkuu hebu nishauri kwa wazo langu

Naweza kufanya hivyo na unahisi changamoto ni nini hasa? Target yangu ni hoho,bamia,nyanya chungu na bilinganga ikiwezekana,

Maximum nataka iwe hekari tatu tu

Kwa uzoefu wako itanigharimu kiasi gani bosi mpaka


Ningekufuata PM ila najua wengi wanataka msaada wa kujua gharama hapa so ukiweka wazi sio mbaya sana
 
Mimi uzoefu wangu ni kwenye hoho
Shamaba kukodi sh 100000,mbegu 585000,kuandaa shamba 1250000 ,kupanda vibarua 60000,mafuta kumwagilia 240000,mbolea kupandia 60000,mbolea kukuzia 50000,Mbolea NPK 60000,Mbolea CAN 50000,madawa 250000,palizi 200000, Kijana wa kazi 300000 gharama hizi zinaweza kupunguwa ama kuongezeka kutegemea na mazingira ulipo na gharama hizi ni kwa mtu aliye na vifaa kama water pump mipira ya kumwagilia na pumps za kupulizia dawa NB KWENYE MBEGU BEI INAWEZA KUPUNGUWA MPAKA KUFIKIA TSH 40000 KUTEGEMEA NA AINA YA MBEGU GANI UTAPANADA
 
Nashukuru sana mkuu
 
Changamoto mkuu ni soko ndy maana tunalima kwa timing mfn ukipanda nyanya ya ikatokea kuanzia mwezi wa 2-4 mara nyingi huwa inabei mfn sasa nyanya debe kuanzia tsh 20000 hoho inayotoka kuanzia mwezi wa 3-7 mara nyingi soko lake halisumbuwi Kwanini hiyo miezi changamoto huwa ni kubwa sana kwa mazao husika ktk kipindi hicho so wakulima wengi hawawezi kupambana na changamoto ktk hiyo miezi hivyo husababisha shortage kubw ktk masoko mengi walio soma uchumi wanajuwa maswala ya demand and supply NB KIPINDI HICHO KADIRIO LA DAWA LINAKUWA JUU
 
nimejifunza kitu...big up sana mleta mada
 
Nataka kulima Pilipili hoho naomba kujuzwa juu ya muda zinaochukua hadi kuanza kuvuna, nitavuna mara ngapi, soko lake likoje, faida zake na changamoto zake. Pia mbegu bora nitapata wapi.
 
Mkoa wa pwani hoho zinastawi? Maeneo ya kibaha au Ruvu naomba maelezo kwa anayejua kuhusu hiki kilimo
 
mbegu gani nzuri ya hoho mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…