Msaada kimatibabu hali imezidi kuwa mbaya

Dogo G

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2018
Posts
1,052
Reaction score
440
Habari waungwana,siku chache hapo nyuma nlileweka uzi humu kuhusiana na rafiki yangu ambaye anasumbuliwa na miwasho sehemu za siri,maeneo ya tumboni,kichwani sometimez na hata miguuni muda mwingine.Nilisoma comment zenu,nikamshauri kama baadhi ya watu walivyodai,moja ya ushauri ilikuwa atumie kitunguu swaumu achanganye na maji kama dose.Alianza kutumia lakini ajabu hivi ninavyozungumza amesema ghafla miwasho imeongezeka tena imeanza katika njia ya haja kubwa tena ni muda woote,anasema ameenda choo kikubwa baada ya kumaliza kutoa haja kubwa kuna maumivu yanatokea mfano wa joto fulani likiambatana na muwasho mkali kwa takribani dk 10 hivi kisha kupoa na kurejea hali ya kawaida.

Ndugu zangu wale tuliobarikiwa ujuzi wa masuala ya kiafya hususani medicak officers ushauri wenu wa haraka maana hali ni mbaya,nimewaza ataweza kuwa na bawasiri but anasema hakuna kile kinyama kinachoning'inia.Hii miwasho ni ugonjwa gani huu?
 
mkuu siumeseme ukweli usaidiwe hata mimi ninayo bawasiri ya ndani miwasho huwa inakuwepo mara1-1 nyama pia hamna ila mimi napata maumivu tu..sana nkiwa nimekaa
 
Huyu ana allergy ya vitu fulani ambavyo anatumia
Inabidi aende hospital maana huko ndio wapo wataalamu.
Inaweza kuwa baadhi ya vyakula vinamkataa
Au anaamini ushirikina maana hamshindwi
 
Kumwambia mwanaume mwenzangu na siyo daktari juu ya shikide kuniwasha na joto kupanda ni swala gumu mno.

Hiyo stori utaipata nikipona na miaka miwili ishapita.
 
Useme ukweli ni wewe nikusaidie na dawa kabisa.. Tena bure

Hata Kwa wale nyayo zinazowaka moto...

Kwakua umedanganya umesema uongo kuwa sio we we unasema Rafiki yako... Basi..ugua pole
 
Uliza tu!
ISIS ,ni me au ke.??..maana kuna uchangiaji unakua kama mwanamke, kuna uchangiaji unakua kam mwanamme.

Au vyote kwapamoja niwewe??

Usiulize nikijua itanisaidia nn, nataka kujua km wee ni Ke nikupige mistari..km we ni me ,niwe nakutag kwenye fursa za wanaotafuta wanaume humu.
 
Useme ukweli ni wewe nikusaidie na dawa kabisa.. Tena bure

Hata Kwa wale nyayo zinazowaka moto...

Kwakua umedanganya umesema uongo kuwa sio we we unasema Rafiki yako... Basi..ugua pole
Weka tu kwa faida ya wengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…