Dogo G
JF-Expert Member
- Jul 6, 2018
- 1,052
- 440
Habari waungwana,siku chache hapo nyuma nlileweka uzi humu kuhusiana na rafiki yangu ambaye anasumbuliwa na miwasho sehemu za siri,maeneo ya tumboni,kichwani sometimez na hata miguuni muda mwingine.Nilisoma comment zenu,nikamshauri kama baadhi ya watu walivyodai,moja ya ushauri ilikuwa atumie kitunguu swaumu achanganye na maji kama dose.Alianza kutumia lakini ajabu hivi ninavyozungumza amesema ghafla miwasho imeongezeka tena imeanza katika njia ya haja kubwa tena ni muda woote,anasema ameenda choo kikubwa baada ya kumaliza kutoa haja kubwa kuna maumivu yanatokea mfano wa joto fulani likiambatana na muwasho mkali kwa takribani dk 10 hivi kisha kupoa na kurejea hali ya kawaida.
Ndugu zangu wale tuliobarikiwa ujuzi wa masuala ya kiafya hususani medicak officers ushauri wenu wa haraka maana hali ni mbaya,nimewaza ataweza kuwa na bawasiri but anasema hakuna kile kinyama kinachoning'inia.Hii miwasho ni ugonjwa gani huu?