Msaada: Kipi ni Chuo kizuri kwa Msc. or MA in Economics nikiwa Bongo?

Mshindo

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2009
Posts
478
Reaction score
186
Wadau,Heri ya mwaka mpya!
Katika harakati za kujaribu kurudi shule (moja ya malengo yangu ya mwaka huu), ninahaha kutafuta shule ya post-graduate yenye walau moja ya sifa zifuatazo kwa mpangilio kwa umuhimu:


  1. Chuo chenye hadhi nzuri (reputable) kinachotoa shahada ya uzamili katika uchumi au inayoelekeana na hiyo
  2. Chuo kinachotoa shahada hiyo/hizo kama evening programmes (Kiwe Dares salaam)
  3. Chuo kizuri cha ng'ambo kinachotoa programe hizo kwa distant learning kwa gharama nafuu

Katika kuhaha nimekutana na hii kwa website ya Mzumbe Dar campus


Sijaweza kupata namn yeyote ya kupata more info juu ya hiyo. Tafadhali mwenye information na uzoefu kwa hilo la mzumbe au hayo hapo juu, share please!
Naamini JF ni zaidi ya vyanzo vingine vya taarifa sahihi.
Wasalaam!
 

Mambo vip mkuu? Niamegraduate last month hicho chuo cha bradford university partneship na mzumbe course ya Msc.Economics and Finance for development.
Ni chuo kizuri sana na unapata access nyingi za books na journeys, madarasa yake yanakuwa jioni, assignments zinafanyiwa assesment kwa kutumia turnit kuepuka plagiarism na faida zingine nyingi kama wanazozipata wanafunzi wakisoma vyuo vya ulaya.
Jipange uombe mwakani if Uko interested ,last month wameanza third cohort kusoma.
More info about bradford let's communicate.
 
Asante kwa ushauri mkuu. Nitajaribu kufanya hivyo hasa kwa Mzumbe, maana hiyo ya SUA nahisi itakua ngumu kufanya kwa namna ninayoitaka ya evening programme (unless iwe na distant learning). Hata hivyo naamini maoni na ushauri wa wadau hapa unaweza kuwa bora kuliko hata ule nitakaoupata nikienda pale. Kuna ihwa vini venye zuf mbalimbal hapa,pamoja na unbiased views.

 
Usiumize kichwa , UDSM ni chuo bora Africa.

 
Kaka jaribu University of London.Wana offer distance course

Wanatoa Msc Finance (Economic Policy).

Fee ni GBP 9960 kwa course nzima.
 
Shukrani sana mkuu! Maelezo mafupi but jut what I needed! Unavyosema nijipange kuomba mwakani inamaana imeshachelewa taya ri kwa mwaka huu?

 
Ukitaka kuwa economist mzuri SUA inatosha, kama unataka cheti tu basi Mzumbe ni kwako.
 

Kuna jamaa humu alikua anasema anaona aibu kusema ana master ya mzumbe!!! Embu pitia huo uzi naiman haupo mbali....ukiupata changanya na za kwako..
 
University of Dar es Salaam ni Bora kama una lengo la kuelimika, Kama lengo lako ni Matokeo Mazuri kwenye Vyeti vyako Nenda Mzumbe University.
 
Hauko seriouz wewe,yani nondo za uchumi unataka kuzisoma katika mfumo wa distance learning?

Ulishawahi kusoma course gani distance learning? Tatizo una project mazingira ya kibongo bongo na kuhisi distance learning ni ishu. .Usimkatishe tamaa distance learning is ok as long as you get it from accredited colleges. .
 
kama unataka chuo ambacho ni reputable Africa kwa Postgraduate ya Economics (iwe masters au PhD) UDSM ni best.

Ila ujiandae kisaikolojia na muda coz wao hawatoi evening class na masomo yao ni magumu balaa, inabidi uwe na background nzuri ya Economics au Maths. na GPA yako iwe fresh (3.5 and above)

ila kama ni evening class jaribu mzumbe, hiyo kozi yao wakishirikiana na Bradford nackia ni nzuri.
 

Mkuu

Jaribu kutembelea University of London External Programmes.

Wanatoa Msc Finance - Economic Policy.

Hii kitu imekaa vizuri.Najiandaa kujiandikisha nikamata cheti cha ukweli.Hii ni kwa distance learning

Vitu vizuri havikosi gharama.Tuition fee ni GBP 9600 kwa course yote.

Ukiwa serious utaweza kumaliza course in 2 yrs but wengine inawachukua miaka 5.

Kazi ni kwako
 

Mkuu

Jaribu kutembelea University of London External Programmes.

Wanatoa Msc Finance - Economic Policy.

Hii kitu imekaa vizuri.Najiandaa kujiandikisha nikamata cheti cha ukweli.Hii ni kwa distance learning

Vitu vizuri havikosi gharama.Tuition fee ni GBP 9600 kwa course yote.

Ukiwa serious utaweza kumaliza course in 2 yrs but wengine inawachukua miaka 5.

Kazi ni kwako.
 
Hauko seriouz wewe,yani nondo za uchumi unataka kuzisoma katika mfumo wa distance learning?
Kwa maana hiyo yule mama Mkuya waziri wetu wa fedha na mambo ya uchumi ana kasoro sababu kasoma degree za masafa?
 
Nashukuru kwa michango yote. Bado napokea mingine mipya ili niweze ku-weigh out. Naamini wapo na wengine wanafaidika na michango yenu. Bless you!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…