Msaada, kisheria hapa nichukue hatua gani?

Msaada, kisheria hapa nichukue hatua gani?

Vangigula

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2015
Posts
852
Reaction score
2,739
Wasalam waungwana na nakutakieni kila lenye kheri kwa mwaka 2023.

Direct kwenye point
Kuna plot tulinunua mkoa mmojawapo wa kaskazini na malipo yalikuwa kwa installments 2.

Baada ya malipo ya awali, ambayo yalikuwa ni kama 2/3 ya malipo yote, tulimuomba mzee aliyetuuzia copy ya hati ya umiliki (umiliki wa kimila na ilitolewa na serikali ya kijiji), akakubali kwa mbinde.

Siku tumeenda kuchukua copy, tulimpitia kwake, then tukaenda nae stationery, tukatoa copy, tukamrudishia. Ila alipotoka pale stationery, yeye alipitilizia msibani na nahisi aliipoteza ile hati huko.

Tarehe ya installment ya pili ilivyofika, kabla ya kumlipa tulimuuliza kuwa atupe hati pamoja na mkataba wa mauziano, akasema hati atatafuta, ila akaprocess mkataba akatupa.

Baada ya kumlipa sasa, kila tukimuuliza anasema ametafuta hajaiona, ila ataendelea kuitafuta. Tulitaka tukirasimishe kiwanja ila sasa:

1. Je, kama kweli hati ya kilmila imepotea, na ndo pekee iliyokuwa inamtambia yeye kama mmiliki halali wa plot, kuna taratibu gani za kufuata ili tubadilishe umiliki toka kwake?

2. Je, naweza pata hati rasmi wilayani bila kuwa na hiyo hati ya kimila? And what are the dangers?
3. Baadae tuliongeza eneo kwa kununua eneo adjacent na lile la mwanzo, ila tunataka hati moja ya eneo lote, la kwanza na la pili, je inawezekana? Na taratibu zake zikoje?

Asanteni
 
Nadhani ungeenda baraza la ardhi la wilaya au mkoa uliopo, hapo utapata usaidizi

Mlifika ofisi za serikali???, Kama ni ndio basi ondoa shaka Cha kufanya mchukue kisha kafanye malipo ya Kodi ya ardhi.

Utasajiliwa kwa jina lako kisha utaomba hati ambayo kuna gharama utazitoa japo sizikumbuki, ngoja wadau waje
 
Asante sana mkuu. Nitaenda huko
 
Nadhani ungeenda baraza la ardhi la wilaya au mkoa uliopo, hapo utapata usaidizi

Mlifika ofisi za serikali???, Kama ni ndio basi ondoa shaka Cha kufanya mchukue kisha kafanye malipo ya Kodi ya ardhi.

Utasajiliwa kwa jina lako kisha utaomba hati ambayo kuna gharama utazitoa japo sizikumbuki, ngoja wadau waje

Nje kidogo ya mada mkuu,mfano kiwanja cha kurithi ambacho hakina nyaraka zozote,je?ni utaratibu gani hutumika ili kupata nyaraka kwa mrithi?
 
Nje kidogo ya mada mkuu,mfano kiwanja cha kurithi ambacho hakina nyaraka zozote,je?ni utaratibu gani hutumika ili kupata nyaraka kwa mrithi?
Mkuu unajua inshu za mirathi siku hizi sizipendi kutokana na usumbufu uliopo.

Kama wanufaika ni wachache wanaeza kubaliana umiliki mfano kuuza?? Kama sivyo wanaeza lipia kodi ya ardhi, wakipata fomu ya malipo.

Ndio waombe hati ambayo itakuja na jina la marehemu Kama aliisajili kutoka kwa mmiliki wa zamani ikiwa tofauti Basi watapewa gharama ili ije kwenye jina la mrithi mpya
 
Back
Top Bottom