Msaada kisheria kuhusu (Fraud) mtu kutumia cheti cha mtu mwingine katika kazi zake

Msaada kisheria kuhusu (Fraud) mtu kutumia cheti cha mtu mwingine katika kazi zake

Mr okra Jefa

Member
Joined
Oct 31, 2016
Posts
6
Reaction score
3
Habari,

Naomba msaada kisheria hili lipoje, mwaka 2020 mwezi wa tano, nilipata ajira katika kampuni moja jijini Dar, nimekuwa nao kwa muda wa miaka 4 mpaka mwaka 2024 mwezi wa 7.

Ile naondoka ndo najua kuna mwamba anatumia cheti changu yupo pori moja hivi na hivyo vyeti alipewa na kampuni yangu na kule yule mwamba anatumia kila details inayonihusu mimi.

Na mpaka sasa hivi naandika haya, huyo jamaa anatumia hivyo vyeti vyangu

Naomba msaada kisheria ipoje na je nianzie wapi katika kudai haki yangu. Ninachoogopa zaidi kwa sasa nilipata kazi serikalini je ikifahamika kuwa vyeti vyangu vinatumika sehemu nyingine itakuwaje kwa upande wangu.?

Asante sana, naomba ushauri wenu wakuu
 
pole kwa changamoto,ila alipataje vyeti vyako? na je unazungumzia original certificate au zipi? je uko na ushahidi kwa hilo unaloshutumu? kama uko na uhakika na ushahidi uko nao nafikiri ni vyema ukafanya kama ulivyoelezwa hapi juu kwa kutoa taarifa polisi kwani ni False Pretences hiyo,pia kama unaweza toa taarifa kwa mwajiri wake.
Kama unaweza tafuta wakili mzuri akusaidie kufuatilia hilo suala kabla ni mapema,maana kama ni hivyo Statutory deduction ambazo zinapelekwa katika serikali zitaonyesha kuwa unafanya kazi sehemu mbili,wakati haiko hivyo na inawezekana mwajiri wako hauruhusu mtu kuwa na ajira mbili.
 
Back
Top Bottom