Msaada kisheria kuhusu mirathi

Msaada kisheria kuhusu mirathi

giraffe

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2010
Posts
630
Reaction score
257
vipi kwa kifo cha mwaka 1998
waweza kufungua kesi ya mirathi
leo?Ni watoto 7wa mama
tofauti,baba mdogo alijichagua
kuwa msimamizi,sisi watoto wa bi
mkubwa tulirithishwa kijijini na
watoto wa bi mdogo mjini
DSM.Kulikuwepo na kiwanja cha
mzee kingine jirani na nyumba va
Dar,dingi mdogo akajimegea
akadai chakwake.
NINACHOKITAKA mali zigawiwe
upya na serikali.
SABABU ZA KUCHELEWA
1.Wadogo zangu wa bimdogo
walikuwa wadogo wanasoma
kupitia kodi ya nyumba,niliona
ningemchangnya bi mdogo.
2.Vitisho vya uchawi kutoka kwa
ndugu.
 
Tafuta pesa kwa nguvu zako achana na hayo mawazo mgando kulilia mirathi tena ya familia maskini.Ila unaweza kwenda mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
 
Tumezoea hivyo kwenye jamii zetu mtu akifa kaacha mali basi tunagawana bila ya kufungua mirathi mahakamani. kwa kuwa mambo wakati fulani huwa shwari basi tunaona kuwa ni sahihi, la hasha siyo sahihi kwa sababu umiliki wa zile mali bado unabakia kuwa ni wa marehemu na yeyote atayefungua kesi baadaye mgawanyo wa awali hautakuwa na mashiko hii ni kutokana na ukweli kwamba mahakama pekee ndiyo yenye mamlaka ya kuhamisha umiliki wa mali toka kwa marehemu kwenda kwa warithi kisheria.
ama kwa kile ulichouliza, kwa mujibu wa The Law of Limitation Act, Shauri lenu linaangukia ktk kipindi cha ndani ya miaka 12 uwe umefungua kesi tokea a date of cause of action. lakini kuna exception ambayo inaeleza, kama ndani ya muda muafaka wa kufungua kesi mlalamikaji/walalamikaji watakuwa disability(unsound, lunatics or minor) basi hicho kipindi cha wao kuwa disability hakitahesabiwa, hesabu itaanzia pale disabilty ilipokomea. hivyo basi uhesabu tokea ndugu zako wafikishe miaka 18 mpaka leo hii miaka 12 haijapita kafungue kesi.
 
asante sana Dunia Tabu,sentensi ya mwisho sijaipata vizuri.
 
sheria inaruhusu kama itatokea muda wa kufungua kesi umekwisha, lakini kuna sababu za msingi zilizo fanya muhusika ashindwe kufungua kesi kwa muda muafaka, muhusika anaweza kumuandikia waziri anayee husika na mambo ya sheria akiomba kuruhusiwa kufungua kesi nje ya muda pia atahitaji kutoa sababu za msingi zilizo pelekea kuchelewa kufungua kesi kwa muda muafaka. wazir akilidhishwa na sababu zako atatoa ruhusa na hivyo kuruhusiwa kufungua kesi. kwa kawaida meshauri yote ya madai yanatakiwa kufunguliwa ndani ya miaka mitatu tangu kosa kutendeka.
 
Lakini kumbuka hili sio kusa ni haki na haki haijalishi miaka mingapi.
 
asante sana Dunia Tabu,sentensi ya mwisho sijaipata vizuri.

nimemaanisha, kwa kuwa sababu ya kutofungua kesi ilikuwa ndugu zako walikuwa wadogo. je, tokea wamefikisha utu uzima (miaka 18) ni muda gani umepita hadi leo hii.
pia unaweza kufuata ushauri wa mdau hapo juu wa kumuandikia barua waziri wa sheria ili uweze kufungua kesi na hatimaye upate haki yako
 
Back
Top Bottom