sheria inaruhusu kama itatokea muda wa kufungua kesi umekwisha, lakini kuna sababu za msingi zilizo fanya muhusika ashindwe kufungua kesi kwa muda muafaka, muhusika anaweza kumuandikia waziri anayee husika na mambo ya sheria akiomba kuruhusiwa kufungua kesi nje ya muda pia atahitaji kutoa sababu za msingi zilizo pelekea kuchelewa kufungua kesi kwa muda muafaka. wazir akilidhishwa na sababu zako atatoa ruhusa na hivyo kuruhusiwa kufungua kesi. kwa kawaida meshauri yote ya madai yanatakiwa kufunguliwa ndani ya miaka mitatu tangu kosa kutendeka.