Msaada kisheria; naweza kuishitaki mahakama kama haitendi haki?

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2012
Posts
3,114
Reaction score
3,541
karibuni wanabodi mnipe msaada wa kisheria.

Naomba niende kwenye mada moja kwa moja.Ikiwa kwa uwezo wa kawaida kabisa nimebaini kuwa mahakama kwa kuelewa au kutoelewa haitendi haki kwa mtuhumiwa, je naweza kuishitaki mahakama hiyo? Wajibu wa awali kabisa wa mahakama ni kutenda haki, hivyo kama mtuhumiwa ametenda kosa la kawaida kabisa, Je mahakama haina uwezo wakumfafanulia mtuhumiwa kama kosa lake linastahili dhamana au halistahili? Kama hali hiyo ikijitokeza, mimi mtazamaji wa pembeni naweza kuifungulia mashitaka mahakama inayotenda hayo?
 
Swali zuri, ngoja na mimi nitafute jibu.

Nimetafuta nimepata kitu kama hiki. In short huwezi kuishitaki mahakama- meaning huwezi kumshitaki Hakimu , Judge hata kama amefanya makosa ya kumkandamiza Lema wazi wazi bila kificho (sisemi Lema amekandamizwa, NO)
Wikipedia, the free encyclopediaJudicial_immunity
 
Mahakama inachukuliwa hatua kwa kukatiwa rufaa ili ikahojiwe na mahakama ya juu yake.
 
Hapa yanahitajika majibu na mjadala wa kisheria sio mambo ya siasa. Wale wa siasa wakae pembeni kabisa
 
Mahakama ndiyo chombo cha mwisho cha kutoa haki.
Lakini kuna kitu kinenishangaza majuzi mahakama ya rufaa kukataa hukumu nyingine ya mahakama ya rufaa kutumika kama rejea ya kesi. Hapo sijui inakuwaje?
 
Mahakama inachukuliwa hatua kwa kukatiwa rufaa ili ikahojiwe na mahakama ya juu yake.
Sawa, lakini kuna wakati unaona kabisa hata mahakama ya juu nayo imefanya mambo yanayo tia shaka kuona kabisa kuna mkono mchafu umepita! Nilifuatilia kwa karibu sana kesi ya kutaka kumpindua Mwalimu Nyerere sikuona dalili kuwa majaji walikuwa wana upande, ilikuwa ni sheria bin haki mwanzo mwisho.Lakini siku hizi mmh
 
Yes unakata rufaa, review, revision! ILA, Judge/hakimu unaweza kumlalamikia kwenye tume ya utumishi wa mahakama.
 
Sawa, lakini kuna wakati unaona kabisa hata mahakama ya juu nayo imefanya mambo yanayo tia shaka kuona kabisa kuna mkono mchafu umepita! Nilifuatilia kwa karibu sana kesi ya kutaka kumpindua Mwalimu Nyerere sikuona dalili kuwa majaji walikuwa wana upande, ilikuwa ni sheria bin haki mwanzo mwisho.Lakini siku hizi mmh
Kwa sasa bado Court of Appeal kuna haki inatendeka. Nina imani nao! Nasikitika, na nilikuwa naongea ka Legend advocate of 1970s , tunajiuliza hawa majaji wa mahakama ya rufaa wakitoka- hawa wa JK (aliowalaumu Lema-siyo wote please) haki itakuwaje Tanzania na watawala ambao inabidi wawe msitari wa mbele kunyoosha mambo wanakanyaga sheria na Katiba. Tutaingia pabaya sana. Nawambia wanangu watafute kazi ulaya, kuna mwaka hapa patalipuka kama trend itakuwa hii.
 
Haki ni Nini ? sijawahi kusikia mtu aliyeshindwa kesi akisema ametendewa haki, haki siku zote kwetu binadamu ni mpaka pale tunaposhinda kesi.
 
Yes mtu rohoni mwake mtu aliyeua anajisemea kuwa nilichopata ni haki yangu mana niliua!
 
Haki ni Nini ? sijawahi kusikia mtu aliyeshindwa kesi akisema ametendewa haki, haki siku zote kwetu binadamu ni mpaka pale tunaposhinda kesi.
Hapana mhalifu kimoyomoyo anajua kuwa alichokipata ni haki
 
Kwa sasa bado Court of Appeal kuna haki inatendeka. Nina imani nao! Nasikitika, na nilikuwa naongea ka Legend advocate of 1970s , tunajiuliza hawa majaji wa mahakama ya rufaa wakitoka- hawa wa JK (aliowalaumu Lema-siyo wote please) haki itakuwaje Tanzania na watawala ambao inabidi wawe msitari wa mbele kunyoosha mambo wanakanyaga sheria na Katiba. Tutaingia pabaya sana. Nawambia wanangu watafute kazi ulaya, kuna mwaka hapa patalipuka kama trend itakuwa hii.
Mkuu Retired, ni ngumu lakini habari ya Prof. Soyinka kuamua kufuta green card yake ni funzo kubwa sana kwetu.
Pia hii habari nyingine inayo trend ni 'light on a tunnel'. Ukimsoma sana Mwalimu Nyerere anasema kazi ya ukombozi haikuwahi kuwa rahisi na haihitaji nguvu tu bali inahitaji akili na upeo (vision) zaidi! Mbezeni Lema kwa sasa.

Untitled-2.jpg
 
karibuni wanabodi mnipe msaada wa kisheria.

Naomba niende kwenye mada moja kwa moja.Ikiwa kwa uwezo wa kawaida kabisa nimebaini kuwa mahakama kwa kuelewa au kutoelewa haitendi haki kwa mtuhumiwa, je naweza kuishitaki mahakama hiyo? Wajibu wa awali kabisa wa mahakama ni kutenda haki, hivyo kama mtuhumiwa ametenda kosa la kawaida kabisa, Je mahakama haina uwezo wakumfafanulia mtuhumiwa kama kosa lake linastahili dhamana au halistahili? Kama hali hiyo ikijitokeza, mimi mtazamaji wa pembeni naweza kuifungulia mashitaka mahakama inayotenda hayo?
Mkuu Jerusalem,
Hii mihimili mitatu ya dola kila mmoja umejiwekea kinga zake. Bunge kupitia sheria ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bungeni, limejikinga kwa kutokushitakiwa kwa lolote litakalozungumzwa bungeni na mbunge yoyote. Serikali kupitia mamlaka ya DPP inaweza kushitakiwa ila kwanza ni lazima serikali yenyewe iyakubali hayo mashiraka, DPP akiyakataa, hawezi kuhojiwa na chombo chochote kama vile Kagoda alivyokwapua bilioni 40 za EPA, DPP akamkingia kifua. Mahakama nayo kupitia kifungu cha contept of the court, uhuru wake hauruhusiwi kuingiliwa na chombo kingine chochote, hata jaji au hakimu asipotoa haki, unaruhusiwa kufuta rufaa mahakama ya juu, lakini sio kuishitaki mahakama as mahakama.

Mahakama ikitoa uamuzi ambao sio wa haki, unashitakiwa kwa mahakama ya juu yake. Ukifika juu kabisa bila kupata haki inakula kwako kama Ile kesi ya Mtikila ya moonbea binafsi.

Pamoja na kinga hizo zote, watendaji wote wa vyombo hivyo wanaweza kushitakiwa kwa kosa lolote la jinai, isipokuwa rais ana kinga ya kutokushitakiwa kwa jinai labda madai.

Lakini hiyo kinga ya rais inahusu utekelezaji wa majukumu ya kirais tuu. Mfano Chadema ingeingia madarakani, ingeweza kumshitaki Mwinyi kwa kuigeuza Ikulu yetu kuwa pango la walanguzi kwa sababu ulanguzi sii miongoni mwa majukumu ya urais.

Wangeweza kumshitaki Mkapa kwa kufanya biashara akiwa Ikulu kwa sababu kufanya biashara sio miongoni mwa majukumu ya urais.

Pia wangemshitaki Kikwete kwa matumizi mabaya ya Madaraka alipotasamehe yale majizi ya EPA kwa sababu mamlaka ya rais kusemehe ni kwa wafungwa tuu waliohukumiwa na sio kuizuia sheria kuchukuwa mkondo wake kwa majizi yale.

Paskali
 
.
Maelezo mazuri na yanayoeleweka kwa mtu wa kiwango chochote cha IQ, asante. Kumbe ndio maana nchi nyingine zili opt kuwa na wafalme tu maana definition ya demokeasia ingewasumbua sana.
 
Lakini kuna kitu kinenishangaza majuzi mahakama ya rufaa kukataa hukumu nyingine ya mahakama ya rufaa kutumika kama rejea ya kesi. Hapo sijui inakuwaje?
Ndugu, hupaswi kushangaa kisheria na kwa mujibu wa misingi ya kesi rejea ama doctrine of precedent, mahakama ya rufaa inaweza epuka kutokutumia maamuzi ya awali (yaliyo amriwa na mahakama ya rufaa). Yapo mazingira ama sababu na moja wapo ni kama maamuzi ya awali yalikuwa per incurrium hapo ndipo mahaka ya rufaa yaweza epuka tumia binding decisions na hivyo Ku depart, hyo ndo stare decisis ama doctrine of precedent...!
 
Lakini kuna kitu kinenishangaza majuzi mahakama ya rufaa kukataa hukumu nyingine ya mahakama ya rufaa kutumika kama rejea ya kesi. Hapo sijui inakuwaje?

High court haiwi bind na hukumu ya high court inakuwa bind na Court of appeal judgement
 
Back
Top Bottom