Wakuu yatupasa tuwe makini sana kwa kweli, sio hao wa mitandao ya simu tu.
Mimi wiki iliyopita nililizwa pesa ndefu tu kwenye a/c yangu ya benki, tena ngoja niwataje ni CRDB
Nikashangaa ghafla napokea sms via mobile phone sim banking, kuwa salio la kiasi hicho xxxxxx limetolewa. Aisee, nilichachawa, nakumbuka ilikuwa mida ya jioni,. Nilitoka mbio hadi benk niliyofungulia a/c. Walikuwa wamefunga ila wapo ndani wanapiga mahesabu.
Nilimsumbua mlinzi, akaongea nao. Mhudumu mmoja akaja akaniambia hebu ahakiki taarifa zangu
Wakaanza ooh, ni kweli inaonesha hela imetolewa kimakosa makao makuu, na maneno kibao, vuta subira itarudi.
Niliwawashia sana, kesho yake asubuhi nikawahi tena, nikataka nionane na meneja, wakaniambia hayupo. Nikawaambia naenda kuwaripoti BOT, nakufungua kesi mahakamani, halafu pia siitaki akaunti yao na mzigo wangu wote wanipe
Mbona siku hiyo hiyo walinirudishia pesa yangu, ila kwa kweli hadi sasa sina imani nao tena
N.B
Siku hizi kuna wafanyakazi kwenye hizi taasisi sio waaminifu kabisa, Mimi nadhani hizo pesa wanazipiga hasa hawa watu wa vitengo vya IT
Sent using
Jamii Forums mobile app