Msaada kisheria: Nini maana ya shauri la kesi kuondolewa mahakamani?

Sagungu 1914

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2016
Posts
938
Reaction score
581
Naomba kujuzwa maana ya shauri la kesi kuondolewa mahakamani,na je kesi inaweza kufunguliwa ten au ndio imeishia hapo?
 
Shauri kuondolewa mahakamani inamaanisha kuwa mlalamikaji na mlalamikiwa wameomba kumalizana nje ya mahakama. Kwakifupi ni kuwa shauri linaondolewa Lakini mkishindwana ngoma inarudi ila kwakufuata process Fulani Fulani.
 
Anayeomba shauri kuondolewa ni nani?
 
Ha
Shauri kuondolewa mahakamani inamaanisha kuwa mlalamikaji na mlalamikiwa wameomba kumalizana nje ya mahakama. Kwakifupi ni kuwa shauri linaondolewa Lakini mkishindwana ngoma inarudi ila kwakufuata process Fulani Fulani.
Iko hivi Kuna jamaa namlalamikia kukatalia kwenye kiwanja changu,Sasa katika mipaka ya kiwanja sikuweka majirani nilicho weka ni ukubwa wa eneo na plot namba pamoja na eneo mgogoro ulipo.

Sasa hakimu kasema ameliondoa shauri mahakamani Kwa sababu sijaonesha kiwanja kinapakana na hakina nani(majirani).
 
Kwa mazingira hayo ni kuwa mashitaka yamekosa mashiko yaani ushahidi usio tia shaka. Sasa hata Kama ingekua mbinguni lazima ushahidi uwepo mfano nyaraka kutoka serikali au waliopima na kutoa hati ya kiwanja.

La zaidi kwakua kakatalia kwenye kiwanja ilitakiwa uwe na mashahidi yaani majirani wa pande zote NNE au uongozi wa mtaa. Shitaka limeondolewa Kwa kukosa vielelezo yakinifu.

Kwa minajili hiyo iwapo utakuwa na vielelezo (supportive evidence) unaweza kufungua Tena shauri lako. Lengo la kuondoa mahakamani ni kuwapa nafasi mlimalize nje ya mahakama na ukijifanya kukomaa inaweza kula kwako.
 
Shauri kuondolewa mahakamani inamaanisha kuwa mlalamikaji na mlalamikiwa wameomba kumalizana nje ya mahakama. Kwakifupi ni kuwa shauri linaondolewa Lakini mkishindwana ngoma inarudi ila kwakufuata process Fulani Fulani.
Sasa hiyo process flani ndiyo mziki kuipata!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…