Msaada kisheria

OK 1

Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
37
Reaction score
18
Habari wakuu.

Naomba kufahamishwa kisheria yafuatayo;

1)Je mawasiliano ya simu yanaweza kutumika kama ushahidi kwa mtuhumiwa aliyetumia simu yake kufanya uhalifu eg kuiba,kutukana?

2)Sheria ipi itasababisha mtuhumiwa kufilisiwa mali zake endapo atapatikana na makosa ya wizi baada ya kuacha kazi?


ASANTENI.
 
Nikianza na swali lako la kwanza, sheria ya ushaidi ya Tanzania (Avidence Act Cap 6) kupitia amendment ya kifungu cha 40 inaruhusu ushahid wa kielotronik kutumika ktk mahakama zetu. ushahid huo unaweza ukawa wa saut iliyorekodiwa, picha za kutembea(video) au picha mnato na ujumbe wa maandishi (sms),taratibu zikifuatwa ushahid huo unakubalika mahakaman.Kuhusu swali lako la pili mtu atashitakiwa kwa kosa alotenda kama matumizi mabaya ya ofisi, rushwa/ufisadi, wizi wa mali ya umma nk. Akitiwa Hatiani Adhabu inaweza kuwa kutaifishwa/kufilisiwa mali yake (forfeture), kifungo, faini nk. kuhusu sheria hata penal code cap 16, imetaja adhabu hiyo.
 


Dunia tabu asante kwa muda wako,nimepata kitu kwenye maelezo yako.
 

cc ISIMBA kwa mwongozo zaidi kwa kesi iliyompata...

Good point kaka..
 
Last edited by a moderator:

Sheria kuijua aman.

utaratibu gani ufatwe hadi huo ushahid wa kieletronic kukubalika kutumika mahakamani?
 
ndugu yangu Marengo90 makampun ya sim yana sera za kumlinda mtumiaji (privacy policy) hivyo nikihitaji ushahid wa sms ni lazima upitie chombo cha hak au usalama kiiamuru kampun husika kuwasilisha kwa hicho chombo mawasiliano yanayotiliwa shaka.
kuhusu picha za kutembea au za mnato lazima wataalam wa kompyuta na ICT wahusishwe kwanza kujua kama picha zilizoletwa si za kutengenezwa (photo manipulation)
na kwa saut ni hivyo hivyo, havipokelewi tu kwa kuwa ww umeleta.
pia kama ni picha au saut halis je zinaendana na kinacholalamikiwa?
KUMBUKA: mahakama kukubali ushahid fulan utumike haina maana ushaid huo tayari umethibisha au kukanusha kinacholalamikiwa, hiyo ni hatua nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…