Naomba ushauri nataka kujua vitu gan vinahitajika kwa ajili ya kiwanda kidogo cha kusindika maziwa na product zake zingine na mtaji ni sh ngapi inabid nitafute maana nataka nianze na iyo ila plan kubwa nataka kudeal na mazao ya kilimo kuyaprocess kwenye viwanda vidogo nitakavyoweza kuanzisha kadiri ya mungu atakavyojalia asante
Kabla ya yote, onana na jamaa wa TFDA ili wakuambie 'sera' zao kuhusu mradi huu.
Maana, unaweza ukawekeza sana, halafu jamaa hawa wakaja kupiga kufuli kiwanda chako.
Jamaa hawa kero sana hawa..!!
Nikweli,pale Sido ukahudhurie mafunzo ya usindikaji,maana hata hao TFDA wanauliza kama mhusika anaelim yoyote yenye cheti kwa kazi hiyo.Asante kwa mawazo yenu ila kuna mtu kaniambia nipitie sido kwamba ndo kila kitu na inakua rahis nikipita huko ni kweli??
Mimi ninavyo jua TFDA au TBS hutoa kibali kwa bidhaa ambayo tiyari imeisha anza kazi, TBS hawawezi kukupa kibali halafu ndo ukaanze kutafuta mitambo even TFDA kwa sababu wanakuja kukagua production yako ndo wakupe kibali, so chakufanya hata ukiwaona watakupatia mwongozo tu na wewe utaanza kazi n then watakuja kukagua kuona kama unafuata mashariti yao ndo sasa upewe kibali rasimi au la.
Huwezi pewa kibali kabla hujaanza productions na TBS hivyo hivyo ni lazima uanze kwanza ndo waje kukagua na wana tabia ya kufanya ukaguzi wa kushitukiza utashangaa gari inafunga break mlangoni kwako, so unatakiwa kuhakikisha walio kuambia unayafuata yote.
Pia ni lazima uwaone kwanza kabla hata hujaanza kujenga hata tofali moja la kiwanda chako.
Jamaa hawa wana taratibu zao za ujenza wa viwanda, na ramani ya kiwanda chako lazima iwe inafuata 'process flow' yao TFDA.
Ukijenga tofauti tu, na wakija kukagua na kukuta 'process flow' sio kama wanavyotaka, wanakufungia kiwanda mpaka utakapo rekebisha jengo..!!!!
Hivyo, lazima uwaone kabla ya kuanza kujenga kiwanda.
TBS nao ni hivyo hivyo, watakwambia jengo lako halikidhi 'viwango' vya kutunza 'afya' ya walaji wa bidhaa zako...!!!!!
Ogopa sana TFDA...!!!!
Nikweli,pale Sido ukahudhurie mafunzo ya usindikaji,maana hata hao TFDA wanauliza kama mhusika anaelim yoyote yenye cheti kwa kazi hiyo.
Na pale SIDO unakuwa umewezeshwa kutambulika kama mjasiriamali mdogo ambayo ni credit kwako pia.
Watu tunashindwa kujua ila pale SIDO ni hazina kubwa sana vijana,sema tu watu tunaona kama hakuna kitu.
Watu wengi wenye kupita pale wanakuwa wanajua njia zote na mbinu zote za biashara husika.Na pia SIDO wana vitengo maalum vya kusaidia wahitimu wao either in group au mmoja mmoja.
Na vote pia nenda SIDO
TFDA ni regulator yeye anajikita katika safety of the product Wakati TBS yeye anajikita katika ubora yaani quality,
Nakubaliana mkuu,ila ukaguzi wao ni uleule wote unafanana,sema tu wewe umeandika kizungu kingi .
Safety of the product na hao wengine quality of the product,sasa ukiangalia ni yale yale tu,wote wanapita katika mchakato mmoja ule ule.
Mtafute mtu aliewahi kufanyiwa ukaguzi na hao wote atakuambia mahitaji yao yanafanana.
Asante mkuu,nitaktafuta,nikifungua Bakery mwakaniKaka,TFDA na TBS ni taasisi mbili tofauti na ziko chini ya wizara mbili tofauti.
TFDA iko chini ya wizara ya afya na ustawi wa jamii na inasghurika na ubora wa dawa na chakula na usalama kwa mlaji LAKINI TBSA ipo chini ya wizara ya Viwanda,Biashara na Masoko yenyewe inashughulika na viwango vya ubora vya bidhaa vyote katika sekta zote
Naweza nikakusaidia namna ya kufuata procedure na kusajiriwa na hawa jamaa.
Asante