Hapo kuna kozi kama ya Ufugaji Nyuki hii inahusika na masuala yote yanayohusu usimamizi wa rasilimali nyuki na teknolojia yake. Hii ni kozi maalum na adimu maana Diploma level inatolewa Tabora pekee na Bachelor level ni UDSM na SUA, unaweza kuajiriwa taasisi mbalimbali za maliasili, mazingira, viwanda, biashara na kilimo. Pia, unaweza kujiajiri kwa kufuga nyuki kuzalisha asali, nta, sumu ya nyuki, maziwa ya nyuki, chavua, uchavushaji wa mazao n.k.
Kozi nyingine ni ya Misitu, huko utajifunza kila kitu kuhusu rasilimali misitu kama vile Forest ecosystems, economics, resources assessment and management na engineering. Na unaweza ukasoma kozi zingine ndani ya hiyo kozi kama vile usimamizi wa wanyamapori na ufugaji nyuki pamoja na tourism. Hii pia inatolewa kwa level ya Diploma Moshi, Arusha, na UDOM, kwa Bachelor ni SUA pekee. Ni kozi muhimu sana na mwajiri mkuu ni Serikali lakini kuna NGOs nyingi sana zinahusika na masuala ya misitu kwa uchache ni WWF, TFCG, IUFRO n.k.
Kozi zote zinafaa sana, ila ukipiga kitabu kwa bidii kutoka ni nje nje.
Zingine kama Utalii na Usimamizi wa Wanyamapori ni kozi za maliasili pia.. Natumaini kuna wataalam wanaweza kuzielezea vizuri pia.
Kila la Kheri.
Pia aione
She Quoted you