Mkuu ada yake ni moto wa kuotea mbali ni kama milioni mbili + ipo hapo bugando alafu uwe ulifaulu physics ina ushindani balaa kwenue kudahiliwa
Ila kama una division one jaribu Benjamin mkapa hospital kuna chuo humo wanaifundisha ila utatuma maombi kupitia NACTE kuanzia mwezi wa 8, 9 au 10 hapo ada ni nafuu tatizo competition na kuingia hapo ni sawa na ngamia kupenya kwenye tundu la sindano
Diploma yake inaitwa radiology
Degree yake inaitwa DIAGNOSTIC RADIOGRAPHY
Yaani uwe mtaalamu wa mambo ya ultrasound x ray CT scan n.k
Ila kwa haraka haraka kulingana na ombi lako nenda VETA KIPAWA kasomee ufundi simu LEVEL 1, 2 &3 Kisha piga TV maintenance una malizia na COMPUTER maintenance
Ada ni kama laki 8 kwa vyote (sina uhakika) muda ni kama miezi 8 au 9
Kila lakheri mkuu