Msaada: Kozi ya Ordinary Diploma in Civil Engineering (DIT) ina mkopo wa HESLB? Taratibu zake zikoje?

Msaada: Kozi ya Ordinary Diploma in Civil Engineering (DIT) ina mkopo wa HESLB? Taratibu zake zikoje?

Joined
Feb 14, 2022
Posts
76
Reaction score
113
Wakuu salama,

Natumai mko wote heri. Nina ndugu yangu wa karibu amefanya maombi ya chuo mwaka huu na katika matokeo ya kwanza (Batch One) amefanikiwa kuchaguliwa kujiunga na Chuo cha Teknolojia cha Dar es Salaam (DIT) kusomea kozi ya Stashahada ya Uhandisi wa Ujenzi (Ordinary Diploma in Civil Engineering) kwa muda wa miaka 3.

Changamoto kubwa iliyopo mbele yetu kwa sasa ni suala la kiuchumi (ada na gharama za kujikimu). Tumesikia kuwa serikali kupitia Bodi ya Mikopo (HESLB) kwa sasa inatoa mikopo pia kwa wanafunzi wa ngazi ya Diploma.

Naomba msaada wa uzoefu wenu kwa maswali haya machache:
1. Je, hii kozi ya Civil Engineering (Diploma) DIT ina sifa na kipaumbele cha kupata mkopo kwa asilimia kubwa?
2. Mchakato wa maombi kupitia mfumo wa OLAMS kwa upande wa Diploma kwa mwaka huu wa masomo ukoje? Kuna vigezo gani vya ziada vya kuzingatia ili maombi yasikataliwe?
3. Je, kuna changamoto zozote za kipekee ambazo waombaji wa mikopo ya ngazi ya Stashahada hukutana nazo tofauti na wale wa Degree?

Na miongozo yoyote ya ziada itakuwa msaada mkubwa sana kwetu ili tuwahi dirisha la maombi kabla halijafungwa.

Ahsanteni sana,
nawasilisha.
 

Attachments

  • Screenshot_20260805-110830.png
    Screenshot_20260805-110830.png
    121.6 KB · Views: 16
Back
Top Bottom