Mkuu dist111
Hongera kwa kufanya biashara. Pamoja na mchango mzuri wa Mkuu lucky
sabasaba, nami napenda kuchangia, chini ya kipengele, ushauri
mwingine wowote, kama ufuatavyo:
Karibu kila mtu huwa anataka kuwa tajiri. Tatizo, wengi wetu hatupo
tayari kulipa gharama (we are not ready to leave the comfort zone) kama
ulivyofanya/ ulivyojitosa (kuthubutu).
Kuna aina kadhaa za umasikini, mojawapo ni umasikini wa fikra/ mawazo.
Tukiuondoa kwanza umasikini huu wa mawazo, ni rahisi kuondokana na
umasikini wa kipato. Hakuna njia ya mkato zaidi ya kupenda kujisomea/
kusikiliza vitabu / machapisho au cd mbalimbali zinazungumzia maisha ya
watu waliofanikiwa au kanuni za mafanikio. Hakuna mbadala.
Mkuu, tafuta vitabu hivi na kuvisoma kwa kuanzia, mapema iwezekanavyo
THE CASHFLOW QUADRANT, THE BUSINESS SCHOOL & THE BUSINESS OF THE
21ST CENTURY vyote vikiwa vimeandikwa na Robert T. Kiyosaki.
Vinapatikana kwenye maduka yafuatayo: Scholastic Bookshop (Mlimani City
& Posta), Dar es Salaam Printers, Saramanda, n.k. Pia, kwa wauza
vitabu stand ya mabasi ubungo vinapatikana.
Ninasema kwa kuanzia, kwa maana kwamba kuna vitabu vingi vizuri (sio vya
Robert Kiyosaki peke yake) lakini vitabu hivi vitakusaidia kukupa
mwanga zaidi juu ya Biashara na Ujasiriamali katika karne hii ya 21,
hasa kwa watu ambao tunakumbwa na changamoto za Usimamizi na Mitaji ya
mawazo ya Biashara zetu bila kusahau Ofisi/Eneo (premisis) la kufanyia
biashara na Stadi /Mbinu za Biashara. Zaidi, vitakupa muongozo mzuri
namna unavyoweza kuutumia muda wako wa ziada (part time) kujenga TIMU ya
watu watakaokuwa wanakufanyia kazi (SYSTEM/ NETWORK) kama ambavyo
Bakheresa, Mengi, Manji, Mkono, n.k walivyo na wanavyoendelea kufanya.
Kwa mawasiliano zaidi, piga 0713 366 473 au 0767 277 223.
KILA LA KHERI WAKUU.