Wadau nilikuwa nataka kukopa milioni 3..., namwachia gari akae nayo mpaka nitakomlipa kwa miezi 2 na rate ya 20%
Sasa huyu jamaa kaniambia nikimwachia gari niwache na kadi yake original, na akaniambia kuwa watu wote
wanaokopesha wanafanya hivyo....
Wadau nilikuwa nauliza kuwa ni sawa? na hapo nitakuwa safe side nikiwacha kadi original ya gari?
kwa nini ukakope mtaani? Yaani umwachie kadi na gari?
Huko mtaani unamwamini kiasi gani?
Kwa nini usikope benki na gari liwe collateral?
Huko benki utawaachia tu kadi original na itatunzwa salama kwenye safe za strongroom zao.....
Kaa ufikirie mara mbili mbili kabla ya kukubali masharti ya namna hii kwenye mikopo. Watu wengi wanadhulumiwa sana bongo hata sababu ya msingi. Wakopeshaji wengi ni wakorofi sana maana wanatafuta faida kwa kila mbinu. Ukiweka dhamana ya kitu chenye dhamani kuliko hela uliyokopa atakuwa anakuombea ushindwe kulipa. Mfano kama unakopa milion 3 halafu unamwachia gari yenye dhamani ya million 6 au zaidi, lazima atafurahi ushindwe kulipa deni ili afaidi gari maana atauza kwa faida kubwa. Uwe makini sana.
Jambo hilo litakugharimu sana.
Siku moja nilikuwa kwenye Gari, na pembeni yangu walikuwapo kin mama wawili na mazungumzo yao yalikuwa hivi "KUNA WATU WANATUMIA NGUVU ZA GIZA/KICHAWI ILI KUPATA MALI ZA WATU. WAMEANZISHA/WANATOA MIKOPO LAKINI WATU WATU WANAO KOPA LAZIMA WAWEKEZE GARI/NYUMBA AU SHAMBA. SASA KUNA MTU MMOJA ALIKOPA 5,000,000/= KWA MASHARTI YA KUWEKEZA MAGARI 3.NA ALITAKIWA ALIPE BAADA YA MIEZI MITATU, LA SIVYO MAGARI YAKE YATACHUKULIWA. yULE MTU KWA KUWA ALIKUWA NA UHAKIKA WA KUPATA PESA ZA KULIPA, ALIKUBALI. BAADA TU YA KUCHUKA ZILE PESA, YULE ALIYEMKOPESHA AKAMUULIZA JE, NI KWELI UTAWEZA KULIPA? JAMAA AKAJIBU NI KWELI NITALIPA.
BAADA YAHAPO, NJIA ZOTE ZA KUPATA KIPATO ZA YULE ALIYE KOPA ZILIFUNGA, NA ALIPOONA ZIMEBAKI SI CHACHE MKATABA HUISHE, ALIONA NI BORA AUZE GARI MOJA KATI YA YALE MATATU ILI ALIPE DENI. SHIDA IKATOKEA KUWA WATEJA WA KUNUNUA GARI HAWAPATIKANI. ILIBAKI WIKI MOJA YA MKATABA, NDIPO AKAENDA KWENYE MAOMBI NA KUELEZA KISA KIZIMA, ALIFANYIWA MAOMBI NA ALIPATA MTEJA WA KUNUA GARI LILE KWA 5,000,000, NA ALIPOMPELEKE MDAI WAKE, AKASHANGAA SANA NA KUMWAMBIA "HAMA KWELI UMEWEZA KULIPAJE, SIKUTEGEMEA KABISA KUWA UTAWEZA KULIPA. KWELI WEWE NI BINGWA NA UMENIWZA.
KUNA WATU WENGI WAMEPOTEZA NYUMBA/MASHAMBA NA VITU VINGINE KWA NJIA HII. KUWA MAKINI.
Nataka mkopo wa muda mfupi.....Benki nimeambiwa wanatoa mkopo wa muda mrefu, na nafikiri pia watakuwa na process ndefu
mkuu hii mimi imewai nitokea kabisa, yani siku nampigia jamaa simu nimpelekee fedha yake, akupokea simu kilichofuata ni msg tu, kwamba zimebaki siku mbili na gari keshapata mteja siku ya kurejesha kama sitapeleka pesa basi anauza, hakuna kuongezewa muda wala nini, kwakuwa watu walikuwa wameshaniambia kwamba jamaa anajiamini wala sikujisumbua kumpigia, siku iliyofuata asubuhi nimedamkia kwake, jamaa anatoka ananikuta mimi nimeshika kijibaasha kangu na namwambia nataka kadi na funguo ya gari yangu, aliniuliza mara kumi kumi nimewezaje kumlipa, baadae ndiyo nikaja sikia kwamba jamaa anatumia nguvu za giza kuwedhulumu waliokopa kwake.
haraka haraka inaponza.....
Benki wala hawachukui muda mradi waverify tra kuwa gari ni lako....
Na muda si tatizo unaweza kuchukua mkopo ukasema utalipa ndani ya miezi 6 lakini ukipata hela ndani ya hiyo miezi miwili unaenda unalipa nz deni unafuta, tena unaweza kuprwa hata mkopo mkubwa zaidi