Msaada: Kuagiza nguo online toka China kupitia Alibaba

Msaada: Kuagiza nguo online toka China kupitia Alibaba

HARVESTER

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2013
Posts
287
Reaction score
243
Nina mpango wa kuagiza nguo za wanawake toka China online kupitia ALIBABA mwezi November, Ninataka kuanza kuagiza pieces 200 kwanza, Ninaomba mnipe uzoefu wenu na ushauri kwa ujumla juu ya mambo yafuatayo

1.Gharama za kusafirisha 200 pieces

2.Clearing agencies wanaoaminika kama nikitumia meli

3. Kodi ya TRA inakuwaje

4.Ninaweza kupata faida nikianza na pieces 200? au mpaka niagize container zima?

5. Je nikitumia DHL nitapata faida?

Ninaomba michango yenu ,mawazo na ushauri nashukuru
 
funga safari uende mkuu...hao Alibaba ni wachina si watu wa kuaminika sana, wana uswahili mwingi tu...wachina wenyewe wa mitandaoni ndiyo kabisa...

...utalizwa mkuu halafu ujute na kama mtaji wako ni mkopo wa bank itakuwa hasara mara mbili....pesa imekwenda na deni la benki unadaiwa ambalo itabidi ulipe kwa njia mbadala.

Online transactions kwa uzofu wangu unaweza kufanya na wazungu au wajapan...wapuuzi wengine kama waarabu, wahindi(nafuu kidogo wahindi), na wachina, si wa kuaminika!

...Wabongo ndiyo kabisaa...weezi watupu wamejipanga kuanzia Asia mpaka Ulaya...hao, waogope kama ukoma!
 
chukua ushauri wa Al Zagawi, usipoangalia utalizwa vibaya.......kwanza china nguo zao ni ver low quality my dear......anyway inategemea na soko unalolenga.........ila ni vema ukaenda mwenyewe......siyo ishu sana kwenda china..........but, ukitaka nguo za ukweli...Italy, Thailand........ndo angalau angalau
 
Ninashukuru mkuu kwa ushauri, itabidi nifuatilie hao wazungu na wajapani
 
chukua ushauri wa Al Zagawi, usipoangalia utalizwa vibaya.......kwanza china nguo zao ni ver low quality my dear......anyway inategemea na soko unalolenga.........ila ni vema ukaenda mwenyewe......siyo ishu sana kwenda china..........but, ukitaka nguo za ukweli...Italy, Thailand........ndo angalau angalau

Ninashukuru mkuu itabidi nifuatilie hao wazungu na wajapani na kama kwenda China minimum niwe na kiasi gani cha fedha za kitanzania mkuu?
 
funga safari uende mkuu...hao Alibaba ni waarabu si watu wa kuaminika sana, wana uswahili mwingi tu...wachina wenyewe wa mitandaoni ndiyo kabisa...

...utalizwa mkuu halafu ujute na kama mtaji wako ni mkopo wa bank itakuwa hasara mara mbili....pesa imekwenda na deni la benki unadaiwa ambalo itabidi ulipe kwa njia mbadala.

Online transactions kwa uzofu wangu unaweza kufanya na wazungu au wajapan...wapuuzi wengine kama waarabu, wahindi(nafuu kidogo wahindi), na wachina, si wa kuaminika!

...Wabongo ndiyo kabisaa...weezi watupu wamejipanga kuanzia Asia mpaka Ulaya...hao, waogope kama ukoma!

Aisee kuna jamaa aliniaminisha hao jamaa ALIBABA ni wazuri, nashukuru mkuu kwa ushauri
 
funga safari uende mkuu...hao Alibaba ni waarabu si watu wa kuaminika sana, wana uswahili mwingi tu...wachina wenyewe wa mitandaoni ndiyo kabisa...

...utalizwa mkuu halafu ujute na kama mtaji wako ni mkopo wa bank itakuwa hasara mara mbili....pesa imekwenda na deni la benki unadaiwa ambalo itabidi ulipe kwa njia mbadala.

Online transactions kwa uzofu wangu unaweza kufanya na wazungu au wajapan...wapuuzi wengine kama waarabu, wahindi(nafuu kidogo wahindi), na wachina, si wa kuaminika!

...Wabongo ndiyo kabisaa...weezi watupu wamejipanga kuanzia Asia mpaka Ulaya...hao, waogope kama ukoma!
Mkuu umenena kwa hasira na uchungu sana, vipi ulisha wahi kulizwa na hao jamaa nini?
 
Alibaba ni kampuni ya mchina.ni kampuni kubwa kuliko hata hao amazoni au ebay na ina partinership na yahoo.
Online kama unalipia kupitia pay pal,hao pay pal hawarealese malipo kwa muuzaji hadi mzigo uwe delivered ndo uwape ok .na kama hukuridhika na mzigo kama wamekutumia matambara unaweza kuurudisha na pesa yako ikabaki kwenye account yako ya paypal.
 
kaka hapa hakuna longolongo sikuizi dunia imeendelea sio lazima uende china, chamsingi agiza mzigo lakini katika malipo tumia pay pal kwani unakuwa umesecure your money, achana na maneno ya kukatishwa tamaa, wanaodhurumiwa ni wale wasio kuwa makini.
 
Mi najua kuwa kupitia alibaba ndio unapata majina ya makampuni na kuwasiliana nao direct au? (Sijawahi kununua ila najua waliopata contacts humo na wapo poa wanapata goods zao na kuwasiliana kama kawa)
 
Nina mpango wa kuagiza nguo za wanawake toka China online kupitia ALIBABA mwezi november,Ninataka kuanza kuagiza pieces 200 kwanza , Ninaomba mnipe uzoefu wenu na ushauri kwa ujumla juu ya mambo yafuatayo

1.Gharama za kusafirisha 200 pieces

2.Clearing agencies wanaoaminika kama nikitumia meli

3. Kodi ya TRA inakuwaje

4.Ninaweza kupata faida nikianza na pieces 200 ? au mpaka niagize container zima?

5. Je nikitumia DHL nitapata faida?

Ninaomba michango yenu ,mawazo na ushauri nashukuru

Mkuu wewe agiza achana na watu wanao katisha tamaa wakati hawajawahi kuagiza hata Wembe, Nimeagiza Kwa mara ya kwanza mzigo wa 10 milioni na mzigo ulifika bila tatizo, Alibaba kwa sasa ni mtandao mkubwa sana na Pato lake limeipiku FB, Wako makini

Naukiwa na wasiwasi kuna kitu kinaitwa Escrow, yaani wewe haulipi pesa moja kwa moja kwa anaye kuuzia unamlpa Escrow au Alipay, hawa ndo watakao mlipa muuzaji pindi mzigo utakapo pakiwa kwenye Meli au Ndege,

Kuna makampuni special yaku inspect ila lazima uwalipe wanakagua ubora na kukuambia nawako makini sana kwa sababu ni kazi yao, vile vile kuna kitu kinaitwa Certificate of Inspection, nacho ni kitu muhimu sana,
 
mkuu usiogope kuagiza mzigo mm uwa naagiza kupitia online naninaupata kama nilivyo agiza ebutembelea hapa www.chinaworldbuz.com mawasiliano yao haya phon no +8613127807205 usiogope rugha we ongeanae kiswahili,kichina niwewe tu jamaa wako poa
 
So jameni, kuna mtu mwenye info zaidi za pay-pal? Jinsi mtu wa chini hapa bongo anavyoweza kufungua account nao!?
 
So jameni, kuna mtu mwenye info zaidi za pay-pal? Jinsi mtu wa chini hapa bongo anavyoweza kufungua account nao!?

Mimi nina account na alibaba, lakini nilitapeliwa. Sikupata mzigo na hera zikapotea. Alibaba wakaniitisha documents zote za malipo na emails ili wafuatilie lakini hakuna walichokifanya. Some win, some lose.
 
mie nimekuwa nikiagiza sana vitu tofauti tofauti na nimekuwa nikivipata katika alibaba/aliexpress na natumia visa card, ukiwa na hizi card haina haja ya kujisajiri paypal kitofauti, may be nikupe expereience yangu nakuangiza nguo nguo, mara nyingi nguo inavyoonekana mtandaoni inakuwa ya kuvutia sana sana ikija haiji vile ulivyotarajia yaani some of them zinakuwa kweli vile,vile ila zingine kwakweli haziwi vile vile hii imekuwa changamoto kwangu ingawa mie ninaagizaga zangu mwenyewe na ndugu zangu na sio za kuuza.
 
Kama mtu hajawahi tumia Alibaba si vizuri kufanya upotoshaji humu, wabongo kwa kupotosha kwa kusikiliza story za kwenye vijiwe vya kahawa hatujambo,

Nisha agiza kupitia Alibaba mara 5 na sijawahi tapeliwa, Ila huku mtaani ni fullu uzushi

big up kwa kututia moyo
 
Ww ni mtu muongo sana kwanini unawakatisha watu tamaa kwa kitu ambacho hujui na wala hutaki kujua nani kakwambia Alibaba ni kampuni ya warabu
 
Sio muongo tu, ni mshamba pia,
Watu tushaagiza product kibao na zinafika safely
 
Back
Top Bottom