Msaada: Kuagiza nguo online toka China kupitia Alibaba


1. Kwa ndege 1kg ni 10USD, kwa meli 1 Cubic metre ni 400USD(ushuru included)
2. Huhitaji agency kwa method #1 niliyokupa (ofisi zao zipo tz unakwenda kuchukua tuu)
3.Kwa ndege unalipa Tshs 70,000 kwa kila 32kg, kwa meli hulipi tena ushuru
4.Faida na hasara inategemea biashara itakavyokuwa
5. DHL ni hasara tuu
 
Kwa wale tupendao kuanza kuagiza na hatujui tuanze vipi kujiunga na tufuatie na kipi,,tuelekezeni kwa hilo,,tunahitaji tuagize bracet na saa
 
mkuu usiogope kuagiza mzigo mm uwa naagiza kupitia online naninaupata kama nilivyo agiza ebutembelea hapa www.chinaworldbuz.com mawasiliano yao haya phon no +8613127807205 usiogope rugha we ongeanae kiswahili,kichina niwewe tu jamaa wako poa
... mbona mamba zinapicha ya whatsapp ya with weusi huku umeandika in ya kichina???
 
Unaagiza vipi? Mi nataka nyuzi za kufumia.zinaitwa hands knitting yarn
I hope tayari una kadi ya benki (Master au Visa card) iliyowezeshwa kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao, kama bado nenda kwa benki yako watakupa fomu utajaza taarifa then utawakabidhi ikiwa tayari utatumiwa ujumbe mfupi kwa njia ya simu kwamba kadi yako imewezeshwa kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao etc
Baada ya hapo fungua akaunti yako na Aliexpress (Find Quality Wholesalers, Suppliers, Manufacturers, Buyers and Products from Our Award-Winning International Trade Site. Wholesale Products from China Wholesalers at Aliexpress.com.) pia utatakiwa kujaza taarifa muhimu ikiwa ni pamoja na anuani yako, ambayo ndiyo itakayotumika once wakikutumia mzigo (kama ni kwa posta). ukikamilisha hilo your good to start shopping with Aliexpress. Nimejaribu kucheck hiyo item yako inapatikana, view attachment
Angalizo: Kwenye mtandao kuna matapeli, so unapotafuta bidhaa yako jitahidi kupata taarifa za muuzaji, mara nyingi mi huwa na target seller mwenye order nyingi, 4-5 stars na pia walau awe na muda wa mwaka mmoja na kuendelea, pia huwa nasoma reviews za wateja walionunua kwake ili kujua kama good seller or not
 

Attachments

  • hand knitting yarn.png
    176.9 KB · Views: 157
Hivi hao wakala wapo hapa nchini? Ili ikitokea umeagiza mzigo usipo fike wao ndio wawajibike..
La sivyo mm acha niendelee kuwa mshamba, siwezi kucheza bahati nasibu pesa yangu..
 
mimi nipo nje ya nchi naona uku watu wengi wanatumia ebay kuagiza vitu na vinafika majumbani kwao bila tatizo,na mm nimeona nijaribu kufanya biashara kupitia Ebay nina mpango wa kuleta kofia (Snapback) Bongo kama pc100 hau 2000,mzigo natuma na ndege. Mzigo kutoka uku kuja Bongo amna tatizo. Wasiwasi wng upo posta ya Tanzania mzigo ukifika ushuru sijui itakuaje!?
 
Kaka, Alibaba siyo waarabu ni kampuni ya tajiri namba moja China (Jack Ma). Kupitia alibaba kuna makampuni kibao mojawapo ni Taobao (ambayo inajishughulisha na kuuza bidhaa online). Unaweza kununua kila kitu pale na wanakuletea hadi nyumbani. Mimi nipo Shanghai (China) hapa huwa natumia sana taobao, jamaa wanakuletea mzigo hakuna wizi kabisa. Tatizo kwetu bongo mambo ya online marketing bado sana, huku unaagiza hadi chakula unaletewa hadi home. Ila sina uhakika kwa huko bongo sababu sijawahi kuagiza nikiwa TZ, na mambo ya kodi, nk inabidi ucheck na tra. lakini gharama za usafiri, insurence, nk huwa zinawekwa ktk mzigo wakati unanunua kutegemea sehemu unapotaka mzigo uletwe.

Lakini pia nakubaliana na wewe swala la wizi ambao upo sehemu yeyote. Hii taobao ni kama ilivyokuwa tradecarview kipindi fulani (ni soko tu la mtandao, ndani wapo wauzaji kibao), matapeli waliingia na walipiga sana watu. Hivyo unatakiwa ujiridhishe na mtu unayefanya naye biashara kwanza. Tatizo Kichina nacho ni shida, na waChina wengi hawajui Kiingereza, angalau Japan wengi wanakijua Kizungu.

Kuhusu kusafiri mwenyewe kwa piece 200, duh!!!! Hiyo nauli Dar-Gwangzhou-Dar mtaji kwisha.
 
 

Ni kweli Kristian nasikia bongo sasahivi KIMENUKA. Hata Airport pale ni shida sana aiseee, mzigo kidogo wanakomaa sana. Chamsingi jamaa ajipange tu aache woga wa mtandao siku hizi ndiyo deal, unapunguza gharama za kusafiri mwenyewe na pia unaokoa muda.
 

poa poa mkuu..
 

Noted....I was less informed by then, I was wrong.

See my posting...2013, yours 2016.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…