Msaada kubadili jina la umiliki wa gari

Msaada kubadili jina la umiliki wa gari

dudupori

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2012
Posts
1,795
Reaction score
1,914
Wakuu heshima kwenu, ningependa kufahamu ikiwa unanunua gari lililokwisha sajiliwa kwa jina la mtu mwingine ni utaratibu gani wa kufuata kuweza kubadili jina la umiliki pamoja na gharama endapo zitakuwepo.
 
Nafikiri unaenda TRA na Mkataba wa mauziano, Kadi ya gari pamoja na TIN yako. Gharama za kubadilisha ni kidogo sana!
 
Na card ya gari (Original) lazima isainiwe na mwenye gari (aliyeliuza), kuna sehemu pale chini, ukienda kwenye ofisi za TRA watakuelekeza.
 
Ndiyo! Mkataba lazima upitie kwa wakili ( mwanasheria) au Hakimu (kwa sisi tunaokaa mikoani ambayo haina mawakili) na siyo serikali ya mtaa. Mimi mwenyewe nimefanya transfer mwezi March, 2014.

Gharama za hawa mawakili au Hakimu ni kiasi gani? Jamaa aliyeniuzia gari kwa sasa yuko mwanza na mimi niko Dar sasa kwa hakimu au wakili ni lazima tuwepo wote??
 
Gharama za hawa mawakili au Hakimu ni kiasi gani? Jamaa aliyeniuzia gari kwa sasa yuko mwanza na mimi niko Dar sasa kwa hakimu au wakili ni lazima tuwepo wote??
Mimi nilimpa bia nne na shilingi elfu 20 cash kwani alinisainia bar! Hata hivyo hakuniomba bali mimi ndiye niliyeridhika kutoa.
 
Na barua toka kwa mwanasheria yenye muhuri wake kabisa.

Hapana sio lazima lowyer.
Makubaliano yaabdikwe kwa maandishi, wakiwemo mashahidi wawili, japo ya kawaida ila iwe professional uwandikaji tu wa mauziano, achukue card ya gari, aende nayo tra, pale kuna form I think Kama sikosei anajaza au tra watamjazia, atapigiwa hesabu pale pale,pengine laki moja tu kufanya hio process Inategemea na thamani ya gari.

Gamba jipya siku hio hio unapewa au next day.
 
Nimepewa....nasisitiza nimepewa gari na rafiki yangu wa siku nyingi... Tatizo kaondoka nchini na sitegemei atakuja hivi karibuni. Ili kunidhihirishia kuwa kanipa gari kama zawadi tuliandikishana vichochoroni na mashahidi watatu ambao wapo hadi sasa. Bahati mbaya ninayoigundua sasa yeye rafiki yangu hakuwa mmiliki wa kwanza lakini kadi bado inalo jina la mmiliki wa kwanza. Taratibu gani nazitumia ili kadi isome jina langu? Tafadhali
 
Back
Top Bottom