DONDOO ZA USAHILI WA WRITTEN KUPITIA MFUMO WA KIDIGITALI
Mtihani unafanyika kwa njia ya kidigitali, cha muhimu unatakiwa ufike kwenye kituo utakachopangiwa siku ya interview mapema kabla ya saa 1 asuhuhi maana huwa kuna heka heka za hapa na pale. Mnaweza kuhamishwa darasa au kupewa maelekezo ya ziada. Kituo ulichopangiwa utakiona kwenye akaunti yako ya ajira portal. Hakikisha unaenda kwenye kituo hicho na si vinginevyo.
Nenda na viambatanisho muhimu la sivyo utazuiliwa kufanya huo mtihani; Hakikisha unabeba
1. Vyeti halisi (original copies) cha form four na form six
2. Cheti halisi cha chuo
3. Cheti cha kuzaliwa
4. Kitambulisho kinachokubalika (NIDA, Pass ya kusafiria, leseni ya udereva au kitambulisho cha mpiga kura)
5. Kama majina yako ya academic certificates na kitambulisho au cheti cha kuzaliwa hayafanani hakikisha unatafuta DEED POLL mapema kutoka kwa mwanasheria au wakili yeyote la sivyo utazuiliwa kufanya mtihani.
Tukirudi kwenye mtihani;
Hakikisha unaijua vizuri email yako na password unayotumia kuingilia kwenye account yako ya ajira portal maana ndio utakayoitumia ku-access mtihani wa written.
Msimamizi ndiye atakaye weka address (URL) ya wewe kuuona mtihani wako, atakupangia komputa ya kukaa ikiwa na Login page (ina sehemu ya kuingiza email na password ileile ya ajira portal).
Ukisha-login, utaona maswali 50 ya kuchagua (multiple choice). Muda wa kujibu ni lisaa limoja (1 hour). Hakikisha unajibu maswali yote kabla ya ku-submit. Unaweza ukachagua jibu na kisha ukabadilisha na kuweka lingine.
Mara baada ya kumaliza mtihani wako, hakikisha unajiridhisha umejibu maswali yote kabla ya ku-submit, kuna panel kushoto itaonesha maswali uliyojibu kwa kuyawekea rangi ya kijani na ambayo haujayajibu kwa rangi ya gray(kijibu). Once ukisha-submit ndio basi huwezi kulog-in tena wala kufanya chochote zaidi ya kusubiri matokeo ambayo utayapata siku hiyo hiyo.
MAMBO YA KUZINGATIA:
Achana na mambo ya kupiga chabo. Maana ule mtihani upo very tricky, swali la kwanza kwako sio la kwanza la jirani yako.
Baada tu ya ku-log in screen ya maelekezo itakuja na itadumu kwa dakika tatu kisha mtihani utakuja. Utakuwa kwenye screen yote. Usije ukathubutu ku-minimize ile screen kwa sababu yoyote ile. Ukifanya hivyo mtihani utaji-submit na utakuwa umeshafeli.
Zingatia sheria zote za mtihani maana ukikamatwa unaibia utafungiwa kufanya mitihani ya PSRS kwa muda usiojulikana pia unaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu.
Simu, saa zote na vifaa vya kidigitali haviruhusiwi wakati wa kufanya mtihani, ukijanavyo utalazimika kuviacha mbele ya chumba cha usaili.
BAADA YA MTIHANI:
Kama uliomba nafasi zaidi ya moja utaendelea kusubiri kwenye chumba cha mtihani ili kufanya interview nyingine mpaka zote umalize.
Baada ya kumaliza mtihani subiri matokeo yako kwenye account yako kama umekuwa SELECTED au NOT SELECTED kwa hatua inayofuata. Marks ulizopata zitawekwa kwenye tovuti ya ajira utumishi kwa namba yako ya mtihani. Mara nyingi majibu hutoka kuanzia jioni maana interview zote zinakuwa zimeshamalizika za siku husika.
Kama kuna jambo sijalitaja wataalamu wengine watatoa mwongozo. Best wishes watumishi wa umma.