Anyway,inaonekana tatizo lako kidogo linahitaji maelezo zaidi ya hayo uliyotoa. Ni kweli kuna conditions nyingi zinazofanya ngozi kubadilika rangi kwawa njano,blue,nyekundu na rangi kufifia(wengine watasema nyeusi),lakini rangi kubadilika kuwa nyeusi kama masizi kukweli inahitaji maelezo ya kina ndugu yangu.
Sikatai ngozi kubadilika kuwa nyeusi,maana kuna conditions nyingi zinazofanya ngozi iwe hivyo ila mara nyingi zinachukua muda mrefu na pengine zinahitaji tiba kabla ya kupotea lakini sio kama hivyo ulivyosema dakika 5.
Sina hakika na rangi ya asili ya ngozi yako,ila kwa watu wenye ngozi nyeupe(natural/artificial) wanapolala wakiamka upande aliolalia uanakuwa hyperpigmented kwa sababu ya kukandamizwa vimishipa vigogo vilivyo chini ya ngozi na kupelekea damu kutosafiri vizuri sehemu ile. Baada ya kuamka hurudi kwenye hali ya kawaida. Lakini pia ikiwa kwa bahati mbaya wakati upo usingizini utalalia mishipa inayopeleka damu kwenye mkono huo uliolalia hali hiyo itatokea,lakini haitakuwa kwenye kiganja tu,itatokea kwenye sehemu yote ya mkono unaohusika. Pia haitahusu mikono yote. Ndio maana nimesema hapa yanahitajika maelezo ya kina zaidi.
Napenda kukumbusha kwamba ili daktari akusaidie unatakiwa kutoa maelezo ya kutosha na very precise. Maana madaktari wanatumia process 2 au 3 hivi kabla ya kupata conclusion(diagnosis)ya tatizo la mgonjwa. Kuna history taking-hapa mgojwa anaelezea in-out ya tatizo lake,daktari anamsikiliza kwa makini huku akijenga taswira kichwani mwake juu ya tatizo hilo.Baada ya mgonjwa kumaliza maelezo yake inafuata hatua ya Clinical examination-hapa daktari anamkagua/anampima mgonjwa.Hapa ndipo daktari anaunganisha alichokiona na maelezo ya mgonjwa kisha anapata jawabu(diagnosis). Lakini inawezekana daktari asione chochote cha maana,hapo ndipo anaingia hatua ya tatu:Laboratory investigations-mgonjwa anachukuliwa vipimo maabara. Majibu ya vipimo yakitoka,daktari anaunganisha majibu hayo na maelezo ya mgonjwa kisha anatoa tiba. Je,ni kwanini nimetoa mlolongo mrefu hivi juu ya nini madaktari hufanya? Pengine unaweza usione umuhimu wake; lakini ninchotaka kuonesha hapa,ni jinsi gani maelezo mazuri ya mgonjwa yanavyohitajika ili kupata tiba nzuri!
Anyway,ushauri wangu kwako ni kwamba:ikiwezekana mtafute daktari mzuri-ukipata daktari bingwa wa magonjwa ya ngozi(Dermatologist) itakuwa vizuri zaidi,kisha mwelezee mwanzo-mwisho juu ya tatizo lako naamini atakusaidia.
Nimalize kwa kukupa pole ndugu yangu.